Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Wankyo Nyigesa, akizungumza na waandishi wa Habari.
................................................
NA
MWAMVUA MWINYI, PWANI.
WATU
sita kati yao akiwemo mtoto mchanga jinsia ya kike ,waliofariki dunia katika
ajali ,iliyotokea kijiji cha Msata, barabara kuu ya Segera /Chalinze mkoani
Pwani ,wametambuliwa majina yao ili ndugu wakabidhiwe kwa ajili ya mazishi.
Akitoa
taarifa za muendelezo kuhusu ajali hiyo, kamanda wa polisi mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Wankyo Nyigesa alisema hakuna
idadi ya vifo iliyoongezeka zaidi ya taarifa iliyotolewa awali.
Alitaja
miili ya marehemu iliyotambuliwa kuwa ni Ibrahim Kilama (28), Mohammed Amir
Shekaoneka (28 mkazi wa Korogwe na Omary Rashid (28) Tanesco Magomeni jijini
Dar es salaam.
Wengine
ni Lihatu Yahaya mtoto mchanga miezi mitatu mkazi wa Handeni ,Hassan Zabuni
kondakta wa gari namba T. 124 DHW aina ya Toyota coaster na Emmanuel
Cosmas (30) mkazi wa Chalinze .
Aidha
Kamanda Wankyo alieleza, watu saba waliopata majeraha kwenye maeneo mbalimbali ya mili
yao , kati yao watano wameruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu na wengine
wawili bado wapo hospital ya Tumbi Kibaha kwa ajili ya matibabu zaidi.
“Ajali
hiyo ilitokea novemba 5, majira ya saa moja usiku baada ya gari namba T. 124
DHW aina ya Toyota coaster ikitokea Mkata kwenda Mbezi -Dar es salaam
,kuligonga kwa nyuma bila kuchukua tahadhari ,lori namba KBV 746C/ZE2861 FAW
iliyokuwa imeegeshwa barabarani kutokana na kuharibika.”
Kamanda Wankyo
alitaja chanzo cha ajali, ni uzembe wa dereva wa gari namba T. 124 DHW aina ya
Toyota coaster kujaribu kulipita bila tahadhari gari jingine lililokuwa
limeegeshwa baada ya kuharibika na wanaendelea kumsaka.
Kutokana na ajali hiyo kamanda huyo alitoa wito kwa madereva, kutii sheria za usalama barabarani na kuacha tabia za kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi ili kuepuka ajali ambazo chanzo chake ni kukiuka sheria za usalama Barabarani.
Kutokana na ajali hiyo kamanda huyo alitoa wito kwa madereva, kutii sheria za usalama barabarani na kuacha tabia za kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi ili kuepuka ajali ambazo chanzo chake ni kukiuka sheria za usalama Barabarani.
Kamanda
wa polisi mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Wankyo Nyigesa, (katkati) akionesha Gari lililopata ajali, kushoto ni
Mkuu wa Polisi Wilaya ya kipolisi Chalinze Mrakibu Mwandamizi wa Polisi
(SSP) Janeti Magomi.
No comments:
Post a Comment