RIDHIWANI APONGEZWA CHALINZE KWA KUTEKELEZA AHADI.
Na Shushu Joel, Chalice. MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amekuwa gumzo jimboni humo mara baada ya kutimiza moja ya ndoto zake alizokuwa akizifikilia kuwatimizia wananchi wake. Ujasili wake na uthubutu wake katika kuhakikisha wananchi wake wa chalinze wanakuwa na neema ndio umepelekea kuwa Gumzo kila kona ya jimbo la chalinze. Akizungumza na wananchi wa kata ya Miono Mbunge wa jimbo hilo aliwahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa hakuna kijiji kitakachorukwa na mradi wa Usambazaji umeme vijijini (Rea). Alisema kuwa wakati anaanza ubunge alikuwa akijiuliza ni lini changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme itamalizika ingawa nilijua kuna siku wananchi wangu wote kuna siku watakuwa nuruni. "Umeme ni ajira hivyo ukitumika ipasavyo utapunguza tatizo la ajira kwa vijana na hata kuchangia kwa ongezeko la pato katika Halmashaur yetu kupitia kuanzishwa kwa fursa mbalimbali kwa kupitia upatikanaji wa ume...