Mtanzania Mohamed Mansour
mkazi wa Kijiji cha Ruvu, Kata ya Ruvu Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, akiwa
katika picha Mara baada ya kimalizika kwa uchaguzi uliomchagua kuwa Rais wa
Chuo Kikuu cha Patrice Lumumba kilichopo nchini Urusi.
........................................
Na Omary Mngindo
UMOJA wa Wanafunzi na
Vijana wa Kiafrika Chuo Kikuu cha Urafiki cha Patrice Lumumba kilichopo nchini
Urusi, wamemchagua Mtanzania Nassoro Mansour kuwa Rais katika chuo hicho.
Uchaguzi huo uliofanyika
mwishoni mwa wiki nchini humo, Mansour ambaye hakuwa na mpinzani, alipigiwa
kura za ndio 23 kati ya 25 hatua iliyotokana na kukidhi vigezo katika mchakato
wa mchujo.
Akizungumza kwa njia ya
simu, Mansour alisema kuwa uchaguzi huo ulioshirikisha mataifa mbalimbali,
Makamu wa Rais wa chuo hicho amechaguliwa Mahamat Muqaddam wa Chad, Katibu Mkuu
Diouf Daur wa Senegal huku
Naibu Katibu Mkuu akiwa amechaguliwa Dju Orlindo automation kutoka Guinea Bissau.
Mansour alisema kuwa,
Patrice Lumumba ni Chuo Kikuu cha Urafiki cha Watu wa Urusi, kilichoanzishwa
mwaka 1960, kikapewa jina la Patrice
Lumumba University
kuanzia 1961-1992.
"Chuo hiki kina
mataifa zaidi ya 155 na tamaduni za watu wa dini zote duniani ambao ni
wastaarabu, pia kina walimu na wahadhiri na maprofesa kutoka nchi mbalimbali
duniani lakini zaidi ni Warusi wenyewe," alisema Mansour.
Aliongeza kuwa nafasi ya
Urais katika chuo hicho inagombewa kila mwaka, na kwamba mgombea hawezi kurudia
tena nafasi hiyo baada ya kumaliza kipindi chake cha mwaka mmoja.
Mansour alisema kuwa yeye
ni Mhadhiri Msaidizi katika chuo hicho, Kitivo cha Uchumi, Idara ya Jiografia
na Uchumi wa Kikanda, pia ni Mwanafunzi wa Stashahada ya Uzamivu na kwamba
ndio mara ya kwanza kushika wadhifa huo.
Ametanabaisha kuwa hiyo
ndio mara ya kwanza kwa Mtanzania kuwa rais katika chuo hicho, kwa mwaka wa
2018/2019 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1960.
"Nimeshika nafasi hii
baada ya Mwanadada Alice Lafara kutoka nchini Madagasca kumaliza muda wake wa
Uraisi ambaye alichaguliwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2017/2018," alisema
Rais hiyo.
Mansour alisema kuwa nchi
zilizopiga kura kumchagua Raisi zilikua 45, kupitia Wawakilishi na Maraisi wa
Wanafunzi wa nchi hizo ambapo waliowania nafasi hiyo walikuwa watatu.
"Mimi ni kijana wa
pili kutoka Afrika Mashariki kushika nafasi hii, aliyetangulia ni Mwanadada
Lilian kutoka nchini Kenya miaka kadhaa iliyopita, nawashukuru walionipogia
kura," alisema Mansour.
Aidha Mansour amewashukuru
wa- Tanzania
wote waliomuombea dua wakati anaingia katika kinyang'anyiro hicho, huku
akimalizia kwa kusema kwamba nafasi hiyo imekua ikishikwa na vijana wa Kiafrika
kutoka Afrika ya Magharibi hasa Nigeria
Mtanzania
Mohamed Mansour aliyefunga Tai akiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wenzake
katika ukumbi wa mkutano wa Chuo Kikuu cha Urafiki cha Patrice Lumumba kilichopo nchini
Urusi.
Pichani wajumbe wa Mkutano
Mkuu wa Uchaguzi wa Chuo Kikuu cha Patrice Lumumba kilichopo nchini Urusi,
wakiwa kwenye ukumbi wa tayari kwa zoezi hill, lililomchagua Mohamed Mansour
kuwa Rais wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment