Posts

Showing posts from November, 2016

MAADHIMISHO YA SIKU YA WALEMAVU KITAIFA YAFUTWA

Image
Maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani, ambayo kitaifa yalitarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam,Desemba 3, mwaka huu yameahirishwa na badala yake kila mkoa utaadhimisha kivyake. Akitoa tamko la kuharishwa kwa maadhimisho hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene amesema maadhimisho hayo yalilenga kila halmashauri isafirishe wanachama wa vyama vya watu wenye ulemavu ili washiriki maadhimisho hayo jijini humo. Amesema kwa mujibu wa maelekezo aliyopewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa wakuu wa mikoa kuwa badala ya maadhimisho hayo ya kitaifa kukusanya walemavu wote kwenye mikoa kwenda Dar es salaam yafanyike kwenye mikoa yao.

HALMASHAURI ZAONGOZA KWA RUSHWA ZIKIFUATIWA NA POLISI.

Image
  Halmashauri nyingi hapa nchini zinaongoza kwa kupokea rushwa kubwa kubwa huku jeshi la polisi likiongoza kwa kupokea rushwa ndogo ndogo suala ambalo limepelekea mapambano dhidi ya rushwa kuwa magumu. Hayo yameelezwa jana na Mkurugenzi wa Takukuru Valentino Mlowola wakati wa mkutano wa mkuu mwaka wa siku 2 wa Shirikisho la mamlaka za kuzuia na kupambana na rushwa nchi za Afrika Mashariki(EAAACA) unaofanyika jijini Arusha ambapo unawashiriki kutoka mataifa 8 barani Afrika. Mlowola alisema kuwa Hadi sasa katika kipindi cha mwaka mmoja wa wameweza kuokoa zaidi ya billion 45 za miradi mbalimbali zilizokuwa ziangukie mikononi mwa watu wachache ambapo aliitaka jamii kutoa ushirikiano dhidi ya mapambano ya kuzuia rushwa. Alisema kuwa miradi mingi inayopitia katika halmashauri nyingi hapa nchini imekuwa ikigubikwa na rushwa na kuifanya miradi hiyo kujengwa chini ya viwango hali inayopelekea matumizi mabaya ya fedha za umma. Aidha katika jeshi la Polisi alitanabaisha k...

ASKARI POLISI AFARIKI DUNIA KIBAHA KWA KUJIPIGA RISASI BILA YA KUKUSUDIA.

Image
Askari   Polisi   mwenye namba H.3348 PC   Armand   Evarist   Furaha mwenye umri wa miaka 33 amefariki dunia baada ya kujipiga risasi kwa bahati mbaya. Taarifa iliyotolewa na   Kaimu kamanda wa   Polisi   Mkoa wa   Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP- Blasius Chatanda imesema tukio hilo   limetokea Tarehe 22 Novemba 2016 majira ya saa moja usiku katika eneo   la maili moja sokoni, kata ya maili moja Tarafa ya Kibaha Wilaya ya Kibaha   mkoani   Pwani. Kaimu Kamanda Chatanda alisema Marehemu alikuwa amepangiwa lindo kwa mkuu wa wilaya ya Kibaha ambapo baada ya kushuka   kwenye Gari   Bunduki ilfyatuka   na   kumjeruhi na   kwamba alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya rufaa ya Tumbi. SSP Chatanda alisema marehemu alikuwa mbele katika Gari namba PT 1732   lililokuwa likiendeshwa na Askari mwenye namba F. 3064 CPL Grayson na kutaja Bunduki aliyokuwa nay...

MAHAFALI SEKONDARI YA YEMEN, WAHITIMU WATAKIWA KUWEKA MALENGO YA KUENDELEA NA MASOMO.

Image
Wahitimu wa kidato cha 4 Shule ya Sekondari Yemen iliyopo Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Benki ya Amana, Dkt. Muhsin Masoud akizungumza katika mahafali hayo. .............................   Vijana waliomaliza elimu ya sekondari   wametakiwa kuweka malengo ya kuendelea na elimu ya juu ili   kuongeza ufahamu   wa mambo mbalimbali katika maisha yao. Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa Benki ya Amana, Dkt. Muhsin   Masoud alipokuwa akizungumza katika mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne katika shule Sekondari yemen iliyopo Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Dkt. Muhsin   ambae alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, amesema Kidato cha nne sio mwisho wa   elimu na kwamba kila muhitimu anatakiwa kujiwekea malengo ya kuendelea na elimu ya   juu. Aliongeza kwa kusema kuwa, sio lazima ukimaliza kusoma ukaajiriwe bali elimu itakufanya uweze hata   kuendesha mambo yako kwa ufanisi. Aidha, a...