Na Alodia Dominick, Bukoba Daktari wa viungo Haruna Ayubu maarufu kama Rubai (63) mkazi wa kata ya Rwamishenyi manispaa ya Bukoba amepandishwa kizimbani kwa shitaka la ubakaji wa mtoto wa miaka 12. Rubai amefikishwa katika mahakama ya wilaya Bukoba Oktoba 23 mwaka huu na kusomewa kesi ya jinai namba 30251/2024. Upande wa mashtaka unaongozwa na mawakili wawili ambao ni Matilda Assey pamoja na Alice Mutungi. Akisoma maelezo ya awali wakili upande wa mashtaka amesema kuwa, kati ya Desemba 2023 na Oktoba 19, mwaka huu mshitakiwa amekuwa akimuingiza mhanga katika moja ya chumba katika ofisi yake iliyopo mtaa wa Pwani, kata ya Miembeni manispaa ya Bukoba. Assey ameeleza kuwa, alipoingia katika chumba hicho alimvua mhanga nguo zake za ndani kisha na mshitakiwa kuvua nguo zake na kuchukua uume wake na kuuingiza kwenye uke wa mhanga baada ya mshitakiwa kumwingilia au kumbaka mhanga amekuwa akimpatia sh. 10,000 au 5,000 kwa ajili ya kuwapelekea wazazi wake. Aidha amesema, Oktob...