Katibu wa mbunge wa viti
maalum mkoa wa Pwani ambaye pia ni Naibu waziri wa Nishai Subira mgalu
akikabidhi vifaa vya ofisi kwa mwenyekiti wa UWT mkoa wa Pwani Farida Mgomi.
..............................................
Na Shushu Joel, Mlandizi
NAIBU waziri wa Nishati Subira Mgalu ambae
pia ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, amemwaga vifaa kwa ajili ya matumizi
ya ofisi kuanzia ngazi ya matawi mpaka kata kwa lengo la barua zote ziwe katika
mfumo wa kiofisi na wepesi wa kutambulika kwa barua hizo kule zitokako kirahisi
Akikabidhi vifaa hivyo katika mkutano wa
jumuiya ya wanawake mkoa wa Pwani uliofanyika katika wilaya ya Kibaha, katibu
wa mbunge huyo Rehema Kawambwa alisema kuwa kutokana na majukumu ya
kitaifa Mgalu ameshindwa kufika lakini uwepo wa katibu ni sawa na kuwepo kwake,
vifaa tumevikabidhi ili viweze kuanza kutumika katika ngazi zote ambazo Naibu
waziri huyo amezilenga kwa ajili ya kupata vifaa hivyo.
“Uwepo wa vifaa katika maofisi yetu ya
jumuiya ya wanawake yatasaidia kupunguza changamoto nyingi lakini kubwa ni
utambulisho wa barua kule zitokako ili hata wanaozipokea waweze kuzitambua kwa
urahisi na kuzifanyia kazi kwa haraka”Alisema katibu wa Naibu waziri wa
Nishati.
Aliongeza kuwa vifaa hivyo vina thamani ya
zaidi ya milioni 2 kwani ni vifaa vingi ambavyo vinahitajika katika kuendesha
shughuli zote za kiofisi ili ofisi iweze kutambulika,kata hizo ni
mtongani,kilangalanga,magimbi, janga,dutumi,soga,book, mlandizi,mtambani
na nyingine zote ikiwa na madhumini ya kuwasaidia wanachama katika utambulisho
wa barua zao zote.
Aidha aliongeza kuwa vifaa hivyo vitakuwa ni
chachu ya kuigwa kwa sehemu zingine hapa nchini kutokana na ofisi nyingi
za chama zimekuwa zikisaulika sana na huku chama ndio kilichoshika
dola,hivyo pia vifaa hivyo vitachangia kuwafanya kinamama kuunda vikundi
na kuwezeshwa kupata mikopo kupitia halmashauri zetu.
Akipokea vifaa hivyo Mwenyekiti wa umoja wa
wanake mkoa wa Pwani Farida Mgomi amesema kuwa Mgalu amekuwa kiongozi wa pekee
katika jumuiya hiyo kwani amekuwa akijitolea katika ufanikishaji wa vitu
mbalimbali kwenye jumuiya hiyo.
Hivyo Mgomi amewataka viongozi wengine kuiga
mfano wa Subira Mgalu ili kuhakikisha jumuia hiyo inakuwa ya kuigwa katika
jumuia zote hapa nchini na hata nje ya nchi.
Aliongeza kuwa kwa kipindi hiki jumuiya ya
wanawake imekuwa ni ya kuigwa kutokana na jinsi jumuiya hiya inavyojitolea
katika ufanikishaji wa maendeleo mbalimbali katika mkoa wa Pwani.
Katibu
wa mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Rehema Kawambwa akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo.
No comments:
Post a Comment