Posts

Showing posts from August, 2022

DC. BAGAMOYO AFANYA KIKAO NA KAMATI YA SENSA WILAYA.

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Zainab Abdallah, akizungumza katika kikao alipokutana na Kamati za Sensa za Halmashauri za Bagamoyo na Chalinze. .................................   Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Zainab Abdallah Amefanya Kikao na kamati ya Sensa ya Wilaya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) ya Wilaya kufuatia maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23/08/2022.   Mkuu huyo wa Wilaya pia ameendelea kuwasisitiza Wananchi wa Bagamoyo, wawe tayari kuhesabiwa Tarehe 23 Mwezi huu itakapofika ili kusaidia serikali iweze kupanga Mipango ya maendeleo kwa Miaka 10 ijayo.   Alisema ili serikali iweze kupanga mambo mbalimbali ya maendeleo inahitaji kuwa na idadi ya wananchi wake iliyo sahihi kwaajili ya kufikisha huduma za jamii mahitaji yaliyo sahihi.   Kikao cha kamati ya sensa kimefanyika ili kufanya tathmini ya mwenendo mzima wa maandalizi ya zoezi la sensa na hali halisi ya mwenendo wa mafunzo ya wata...

RC KUNENGE AMEITAKA NDC KUANDAA MCHORO ENEO LA KONGANI YA UWEKEZAJI KIBAHA KWA AJILI YA KUVUTIA WAWEKEZAJI

Image
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani   MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amekutana na uongozi wa Shirika la Maendelo la Taifa – NDC kwa mazungumzo ya kuitangaza Kongani ya Viwanda inayomilikiwa na Shirika hilo, Mjini Kibaha na kuhakikisha inaandaa mchoro wa eneo hilo kwa ajili wawekezaji.   Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa huo ambapo Kunenge amemshauri Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Nicolaus Shombe  kuhakikisha ofisi yake inaandaa mchoro huo ili kuinua uwekezaji.   “Ni wajibu wangu kuzisemea taasisi zote zilizopo mkoani kwangu, hivyo mnapaswa kuandaa mchoro wa eneo hilo, mnipatie ili tuweze kulitangaza kwa wawekezaji wanaotafuta maeneo ya uwekezaji,” alisema Kunenge.  Akifafanua faida za uwekezaji, Kunenge ameeleza kuwa unasaidia katika kufanikisha malengo ya mkakati mkubwa wa mkoa uliolenga kuongeza vyanzo vya mapato, hivyo eneo hilo la NDC ni muhimu na litasaidia kuongeza mapato.   Katika Hatua nyingine, amewapo...

RAIS SAMIA AWATAKA VIONGOZI KUWAHUDUMIA WANANCHI

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Njombe katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba Mkoani humo tarehe 10 Agosti, 2022. ******************************  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imezuia kukata na kupandisha hadhi maeneo ya utawala kwa sababu yanaongeza gharama kwa Serikali. Rais Samia amesema hayo leo wakati akihutubia wananchi wa Njombe katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba. Aidha, Rais Samia amesema mwelekeo wa Serikali ni kunyanyua hali ya uchumi wa nchi ili kuinua hali ya maisha ya mwananchi mmoja mmoja.   Rais Samia pia ametoa wito kwa Viongozi nchini kusimamia ipasavyo miradi inayotekelezwa na Serikali ili kuwajengea fursa Watanzania kufanya shughuli za maendeleo na kuinua kipato. Vile vile, Rais Samia amewataka Viongozi wa Kata, Wilaya na Mikoa kuhudumia wananchi na kutatua kero zao...