Waziri wa nchi Ofisi ya
Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo
kushoto akimpatia maelezo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya
Kisarawe Mussa Gama katika halfa hiyo ya makabidhiano ya mashine kwa
ajili ya kutia magonjwa mbali mbali.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
...............................................................
VICTOR MASANGU, KISARAWE
WAZIRI wa nchi Ofisi ya
Rais Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amekemea
vitendo vya upokeaji wa rushwa vinavyofanywa na baadhi ya
wauguzi,wataalamu wa afya na madaktari kuwataka kuachana na tabia ya
kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wahakikishe wanatoa huduma ya matibabu
kwa wagonjwa kwa kuzingatia misingi ya weledi ya kazi yao bila kuwa na ubaguzi
wowote.
Jafo alitoa kaul
hiyo wakati akizungumza na wataalamu wa afya, pamoja na wananchi wakati
wa sherehe za kukabidhi mashine maalumu kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa ya
aina mbali mbali katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambapo viongozi wa
serikali madiwani pamoja na viongozi wa dini waliweza kushiriki katika zoezi
hilo.
Aidha Waziri Jafo
alibainisha kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha
inaboresha sekta ya afya kuanzia ngazi za maeneo ya vijijini kwa kuongeza
ujenzi mpya wa zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali lengo ikiwa ni
kuwaondolea adha wananchi katika suala zima la upatikanaji wa huduma ya
matibabu kwa urahisi zaidi.
“Napenda kuchukua fura hii
kuwambia ndugu zangu wananchi wa Kisarawe kwa kweli Rais wetu anafanya kazi
kubwa sana ya kuhakikisha analeta maendeleo katika sekta mbali mbali hapa nchini
na kwa sisi watu wa kisarawe tumepata bahati kubwa sana, kwa hiyo nipende
kuwaambia tutaendelea kuboresha huduma ya afya katika zahanati zetu, vituo vya
afya pamoja na ujenzi wa Hospitali nyingine mpya,”alisema Jafo.
Pia Jafo aliupongeza
uongozi wa hospitali ya Wilaya hiyo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa
kusirikiana kwa hali na mali
mpaka kufanikisha kununua mashine hizo za kisasa ambazo zitaweza kutatua
changamoto za wananchi ambao hapo awali walikuwa wanapata usumbufu mkubwa
kuwenda kupata vipimo katika maeneo mengine.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya
ya Kisarawe Jonathan Budenu alisema hospitali ya Wilaya awali
ilikuwa inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa
vifaa tiba pamoja na upungufu wa watumishi kwa asilimia 36 huku
akibainisha wamefanikiwa kununua mashine maalumu za uchunguzi wa
magonjwa ambazo zimegharimu kiasi cha shilingi milioni 119 fedha ambazo
zimetokana na makusanyo ya ndani ya hospitali hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya
Kisarawe Jokate..amesema ataendelea kushirikiana bega kwa bega na
viongozi wengine kwa lengo la kuweza kuwaletea mabadiliko chanya ya
kimaendeleo wananchi wake hususana katika kuwaboresha huduma zaidi ya
afya katika zahanati,vituo vya afya na kuongeza kuwa mipango waliyonayo
ni kuifanya hospitali hiyo kuwa sehemu ya mfano katika
nchi nzima.
“Jambo hili kwetu lina
umuhimu mkubwa sana katika kuwaboreshea wananchi
wetu huduma ya afya na kikubwa ni hapa tunamuunga Rais wetu Dr.John Pombe
Magufuli katika kuhakikisha sekta ya afya inaboreshwa kwa kiwango cha hali ya
juu ikiweo kununua vifaa tiba mbali mbali kama
tulivyofanya katika hospitali yetu ya Wilaya kwa hiyo ni hatua kubwa”alisema
Jokate.
Katika hatua nyingine
Jokate amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanajiunga katika bima ya
afya ambayo itaweza kuwasaidia kupata matibabu kwa urahisi na kuondokana na
kero ya kusumbuka kutibiwa pindi wanapokwenda hospitalini.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe
Jokate Mwegelo akizungumza na wananchi hawapo pichana pamoja na wauguzi na
madaktari katika halfa ya kukabidhiwa rasmi mashine maalumu kwa ajili ya kutibu
magonjwa mbali mbali katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe..(PICHA NA VICTOR
MASANGU)
Waziri wa chi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kulia Selemani Jafo akikata utepe wakati wa sherehe ya kukabidhi mashine kwa ajili ya kutibu magonjwa mbali mbali katika hospitali ya Kisarawe, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mganga mkuu wa Wilaya ya
Kisarawe kulia Jonathan Budenu akifafanua jambo kwa Waziri wa nchi Ofisi ya
Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo mara baada ya
kukabidhi mashine hizo katika hospitali ya Wilaya. (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Waziri wan chi ofisi ya
Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kulia wakiwa
na baadhi ya viongozi wengine wa serikali wa kati kati ni Mkuu wa Wilaya ya
Kisarawe Jokate Mwegelo na kushoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri
ya Kisarawe Musa Gama katika hafla hiyo ya makabishiano ya mashine za kutibu
magonjwa mbali mbali. (PICHA NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment