NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
TAASISI ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa Mkoa wa Pwani, imemfikisha mahakamani Romani Michael Jovin
ambae ni (volunteer surveyor )wa DAWASA kwa kosa la kuomba rushwa ya
sh.70,000 na kupokea rushwa ya kiasi cha sh.50,000 .
Mtumishi huyo amejikuta
akifikishwa kizimbani baada ya kwenda kinyume na kifungu cha 15(1) (a) cha
sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba. 11 ya mwaka 2007.
Romani Michael ambaye
alifunguliwa kesi ya jinai mamba 140 ya mwaka 2018 ni volunteer Surveyor DAWASA
Ubungo.
Akisoma mashtaka hayo
mbele ya hakimu mkazi wilaya ya Kibaha mheshimiwa Herieth Mwailolo, mwendesha
mashtaka wa TAKUKURU, Prisca Mpeka aliieleza mahakama kwamba mshitakiwa
alitenda kosa la kuomba rushwa ya sh.70,000 na kupokea rushwa ya sh. 50,000
kutoka kwa mtoa taarifa ili aweze kumsaidia mtoa taarifa kupata mita ya
DAWASA.
Alisema, jambo hilo ni kosa kisheria
kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa,
sheria namba 11 ya mwaka 2007.
Aidha Prisca aliieleza
,mahakama kwamba mshitakiwa alipokea rushwa ya kiasi cha sh.50,000 kutoka kwa
mtoa taarifa, jambo ambalo pia ni kosa kisheria kinyume na kifungu cha 15
(1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa, namba 11 ya mwaka
2007.
Mshitakiwa alikana makosa
yote mawili na dhamana iko wazi, hata hivyo mshtakiwa ameshindwa kutimiza
masharti ya dhamana na hivyo kupelekwa magereza hadi atakapotimiza masharti ya
dhamana.
Kesi hiyo itatajwa tena
tarehe 27/11/2018.
Kamanda wa TAKUKURU mkoa
wa Pwani, Suzana Raymond anaendelea kuwaasa wananchi wote kufuata taratibu
kanuni na sheria za nchi ili kuweza kwenda na kasi ya awamu ya tano chini ya
Raisi dk. John Magufuli.
No comments:
Post a Comment