Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Pwani Farida Mgomi akizungumza na viongozi wa umoja huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Pwani Farida Mgomi akisisitiza jambo kwa wajumbe wa mkutano huo.
.................................................
Na shushu
Joel,Mlandizi.
MWENYEKITI
wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kupitia chama cha mapinduzi CCM
mkoa wa Pwani Farida Mgomi amewataka wanawake wote katika mkoa huo kuacha majungu,fitina
na chuki na badala yake amewatak kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu kwa
viongozi wao ili kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola nchini kwa zaidi ya
miaka 50 ijayo.
Wanawake
walio wengi wamekuwa wakiendekeza majungu katika jumuiya na kuacha kufanya
kazi za wanachama kwa kuhamasisha uhai wa jumuiya hiyo.
Akizungumza
na wanawake wa wilaya ya kibaha mwenyekiti huyo aliwataka wanawake kuacha tabia
za kinafiki na matokeo yake wapige kazi za uzalishaji kwa ajili ya kutimiza
adhima ya serikali ya awamu ya tano kwenye kuhakikisha nchini yetu inakuwa
katika uchumi wa kati kupitia uanzishwaji wa viwanda.
“Kama kuna
mwanamke ajisikii kufanya kazi na umoja wa wanawake ni bora akajiengua na
kutuachia chama chetu kisichohitaji majungu wala fitina za aina yeyote ile
hivyo ni bora wanafiki wakajiondoa wenyewe bila kufukuzwa katika jumuiya
hiyo”Alisema Mgomi.
Aliongeza
kuwa uchaguzi ulishakwisha kupita hivyo kila mmoja anapaswa kuwaheshimu
viongozi waliopo madarakani na si kutengeneza makundi ambayo hayana tija katika
chama.
Aidha
alisema kuwa wanawake ni msingi mkubwa na wenye kutumainiwa katika chama hivyo
hakuna sababu ya kuendekeza fitina wala majungu katika jumuiya kwani
yatawasambaratisha na kupoteza dira ambayo wamejiwekea katika kukuza uchumi wa
viwanda kwenye mkoa wa pwani.
“Wanawake
wenzangu tutumie fursa zilizopo katika mkoa wetu wa pwani ili tuweze kujipatia
fedha za kuendeshea maisha na familia zetu kwani serikali inatoa mikopo
ya bila riba kupitia halmashauri zetu kote nchini”
Aliongeza
kuwa migogoro imekuwa ikichangia kutoendelea kwa jumuiya nyingi hivyo kutokana
na nafasi yangu ya umwenyekiti wa Uwt sihitaji kuona wala kusikia
chembechembe wala harufu ya mgogoro kwenye jumuiya yangu kwani migogoro
inarudisha nyuma maendeleo ya chama chetu.
Kwa upande
wake Tatu Haji ambaye ni mwenyekiti wa Uwt kata ya mlandizi vijijini
amempongeza mwenyekiti wa jumuiya hiyo kwa jinsi anavyijitolea katika ujenzi wa
jumuiya kwani baadhi ya watu wasio na nia njema na viongozi kuanza kupenyeza
chuki kwa wananchama ili wachukiane.
Aidha
amemtaka mwenyekiti huyo kuongeza ukali wa kuwafukuza au kuwasimamisha
uanachama wale walio na nia ya kuitaka jumuiya kusonga mbele na kuwa ya mfano
katika jumuiya zote za chama.
Naye Lucy
Zebedayo amesema kuwa chanzo cha migogoro mingi inayokuwepo katika jumuiya ni
baadhi ya watu kuwa na tamaa ya kutaka nafasdi za watu ambazo uanza kupandikiza
chuki na fitina na hivyo kupelekea kutengenezeka kwa majungu yasiyo na maana
katika nyadhifa.
Hivyo
aliongeza kuwa ili vitu hivi viondoke katika jumuiya zetu ni lazima viongozi
wetu wafanye maamuzi ili kunusuru juiya zetu,tena ni kwa kuwafukuza watu
uanachama au kuwasimamisha.
“Walio na
nia mbaya na uongozi wetu ni bora wakaondoka kwenye chama chetu mapema ili
pumba na mchele uweze kujulikana”Alisema.
Baadhi ya wajumbe wa
mkutano wa UWT Mkoa wa Pwani, wakimsikiliza mwenyekiti wao wa mkoa kwa makini wakati
akizungumza nao kuhusu wasaliti wa chama kujiengua.
No comments:
Post a Comment