PROF KABUDI ZIARANI FALME ZA KIARABU
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Umoja wa Falme za kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan,Abu Dhabi,Umoja wa Falme za Kiarabu. June 30,2019. Tanzania na Nchi ya Falme za Kiarabu zimekubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika masuala ya usalama wa eneo la Ghuba na bahari ya Hindi pia kusaidia kuimarisha hali ya usalama katika nchi za Somalia na Sudan. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Umoja wa Falme za kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan,Abu Dhabi,Umoja wa Falme za Kiarabu. June 30,2019. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili...