Posts

Showing posts from December, 2023

RMO KAGERA ATENGULIWA KWA KUZUILIWA MWILI WA MTOTO MCHANGA KWA MADAI YA DENI LA MATIBABU HOSPITALINI.

Image
  Na Alodia Babara Bukoba. Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amemwagiza katibu mkuu wa TAMISEMI nchini kutengua nafasi ya mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Issesanda Kaniki baada ya hospitali ya rufaa ya Bukoba ya mkoa huo kuzuia mwili wa mtoto mchanga kwa muda wa siku mbili kutoruhusiwa kwenda kuzikwa wakati wakijua watoto wanatibiwa bure. Maagizo mengine ameyatoa kwa viongozi wa serikali, siasa na watumishi mbalimbali nchini. Waziri Mchengerwa ametoa maagizo hayo  Desemba 15, mwaka huu wa 2023, wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kagera katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani kinachokarabatiwa ambapo pia alishuhudia utiaji wa saini ya mikataba ya usanifu miradi ya uboreshaji wa miundomninu ya miji Tanzania (TACTIC) kwa miji 15 ya kundi la pili. Ameagiza katibu mkuu TAMISEMI kwa kushirikiana na sekta ya afya kufanyika mapitio ya menejimenti nzima ya hospitali hiyo na kutoa maamuzi kwani alipata malalamiko ku...

POLISI KAGERA WAKAMATA SILAHA 11. NA RISASI 115.

Image
  Na Alodia Babara Bukoba. Jeshi la polisi mkoani Kagera limekamata silaha 11 zikiwemo bunduki 2 aina ya AK 47 zikiwa na magazine tatu, risasi 115, bastola aina ya glock 17 na bunduki aina ya gobore. Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP. Blasius Chatanda, akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 14, 2023, amesema kuwa, jeshi hilo  linaendelea kufanya oparasheni mbalimbali na kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi katika mkoa huo ambapo katika oparasheni iliyofanyika kuanzia Septemba, 2023 hadi sasa silaha 11 zilikamatwa. “Katika kudhibiti matukio ya utekaji  nyara hasa kwa wafugaji katika mkoa wetu wa Kagera tumefanikiwa kukamata watuhumiwa 14 wa utekaji, tumekamata silaha mbili aina ya AK 47 zikiwa na magazine tatu pamoja na risasi 115 na bastola aina ya grock 17” amesema Chatanda. Aidha amesema katika kudhibiti matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha na ujagili jumla ya bunduki nane aina ya gobore zimekamatwa na kati ya hizo nn...

WAHITIMU ADEM WAPEWA SOMO NA PROF. MKENDA.

Image
  Wahitimu katika chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa elimu ­(ADEM) wametakiwa kwenda kusimamia vyema taaluma ya uongozi na utawala katika maeneo yao ili kutimiza malengo ya serikali katika maboresho ya elimu hapa nchini. Katika Mahafali ya 31 ya waahitimu hao yaliyofanyika tarehe 01 Desemba 2023, mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema katika kipindi hiki cha mageuzi ya elimu, serikali inawategemea sana walimu hasa waliosomea uongozi na utawala katika kuhakikisha yale yote yanayotakiwa kuboreshwa yanasimamiwa  ipasavyo. Amesema tayari serikali inaendelea na mchakato wa maboresho ya elimu nchini kwa kuangazia mambo saba muhimu ambayo ni sera ya elimu, mabadiliko ya sheria ya elimu ya mwaka 1978 ambapo sasa elimu ya lazima ni miaka 10 kwa kila Mtanzania. Prof. Mkenda ameongeza kwa kusema kuwa, katika maboresho hayo , kuna marekebisho ya mitaala, kuwa na walimu, wakufunzi na wahadhiri kwa mgawanyo uliokuwa sawa,...