Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda akizungumza leo Novemba 14, 2018 Mkoani Lindi.
..........................................................
NA HADIJA OMARY-LINDI
Serikali Nchini Tanzania
imetoa wiki mbili kwa Kampuni au Taasisi zinazomiliki viwanda
vilivyobinafsishwa na serikali bila kuviendeleza ama kubadilisha matumizi
viwanda hivyo kuwasilisha mipango mikakati wizara ya viwanda, ya kuviendeleza viwanda hivyo kabla ya serikali haijachukuwa hatu dhidi yao
Kauli hiyo ya Serikali
imetolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda
alipofanya Zihara ya siku moja katika Mkoa wa Lindi ambapo aliweza kukagua kiwanda
kinachotarajiwa kubangua korosho cha Bucco kilichopo manispaa ya lindi pamoja
na ghara la kuifadhia mazao la Ilulu Wilayani Nachingwea
Kakunda amesema katika
kulisimamia jambo hilo kama Wizara tayari ameshamuagiza katibu Mkuu wa
viwanda bihashara na Uwekezaji kuandaa taarifa ya uchambuzi
kwa Nchi mzima ili kubaini viwanda vyote vidogo, vikubwa na
vyakati kwa vile vilivyobinafsishwa ili kubaini kama vinafanya kazi yake
ya msingi iliyokusudiwa
Alisema kuwa baada ya
taarifa hiyo kuwasilishwa Wizarani itapitiwa ili kuona ni
Viwanda vipi vinafanya kazi iliyokusudiwa na vipi vilivyobadilishwa matumizi
ambapo vile vitakavyobainika kuwa vimebadilishwa matumizi ama
kutoendelezwa hatua za haraka zitachukuliwa na serikali ya kuona
viwanda hivyo vinaendelezwa
“natoa taadhari kwa mtu
yeyote ama kampuni yoyote ambayo ilichukuwa kiwanda akabinafsishiwa
, kilikuwa cha Serikali sasa kimekuwa cha binafsi huyo mtu au kampuni
tangu alipopewa kazi hiyo na akaacha hiyo kazi ya msingi akafanya kazi nyingine
, kama serikali watu hao tunawafanyia kazi
Akizungumzia juu ya
urejeshwaji wa kiwanda cha Bucco Naibu waziri wa kilimo Innocent
Bashungwa alisema kuwa serikali ilipoamua kiwanda hiko kukikabidhi kwa
jeshi la kujenga taifa (JKT) nia ilikuwa ni kuiongezea thamani
korosho ndani ya nchi kutoka moja kwa moja kwa wakulima ambapo inaweza
kukuza pato la taifa pamoja na kuleta ajira kwa wananchi wake
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa
wa Lindi Godfrey Zambi alisema kuwa kiwanda hiko cha Bucco toka kubinafsishwa
kwake kutoka kwa serikali kiliweza kufanya shughuli ya ubanguaji wa korosho kwa
mwaka mmoja wa 2007 hadi 2008 pekee hata hivyo alisema kuwa baada ya hapo
kiwanda hiko kiligeuzwa ghara la kuifadhia korosho mpaka hivi sasa
No comments:
Post a Comment