Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Uwominyi
wilayani Kilolo mkoani Iringa juu ya mikakati ya serikali ya kutekeleza miradi
mbalimbali ya umeme.
..............................
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amebainisha
kutoridhishwa na namna Kampuni ya Mkandarasi Sengerema inavyotekeleza miradi ya
REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza na
kuitaka hadi ifikapo Desemba 15 kuwepo na mabadiliko ya kazi walizofanya katika
Wilaya ya Kilolo.
Mgalu ametoa kauli hiyo akiwa kwenye ziara ya
kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Alisema Serikali ilishatoa maelekezo na
walikubalina na wakandarasi kuhakikisha kila wiki wanawasha umeme katika vijiji
3 na kampuni ya Sengerema imepewa kazi ya kufikisha miundombinu ya umeme katika
vijiji 145 Mkoa mzima na kwa Kilolo ni vijiji zaidi ya 40.
“Muda umebaki mchache wa kukamilisha miradi hii
maana inatakiwa kumalizika Juni mwakani, huku tukiwa tunashuhudia uhitaji
mkubwa wa nishati ya umeme ingawa wigo wa mkandarasi ni mdogo lakini katika
mkataba mkandarasi anaweza kuchepusha kwa asilimia 15.
Alisema tayari wana taarifa ya baadhi ya vijiji na
vitongoji ambavyo vimerukwa na sasa wanafanya uchambuzi baada ya kupokea
taarifa kutoka mikoa yote na kuwa tatizo hilo litaanza kutatuliwa mapema
mwakani baada ya kuanza kutekelezwa miradi ya Ujazilizi, kufikia miji inayokuwa
kwa kasi.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Uwominyi
wilayani Kilolo mkoani Iringa juu ya mikakati ya Serikali ya kutekeleza miradi
mbalimbali ya umeme.
No comments:
Post a Comment