TAASISI YA JAI YAWAFARIJI WAGONJWA KWA MISAADA, SHEIKH MKOA SINGIDA ANENA MAZITO.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro akimuombea dua mmoja wa wagonjwa aliyelazwa kwenye hospitali hiyo. ............................................... Na Dotto Mwaibale, Singida SHEIKH wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro amewaongoza wanajumuiya wa Taasisi Jamiyatul Akhlaaqul Islam (JAI) kwa kuwapatia msaada wa chakula na vinywaji wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Mandewa. Taasisi hiyo ambayo inajihusisha kutoa huduma kwa wagonjwa na yatima imetoa misaada hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Sikukuu ya Eid Al-Adha ilyofanyika leo. Akizungumza kabla ya kutoa msaada huo, Sheikh Nassoro alisema jambo linalofanywa na taasisi hiyo ni jambo jema kwani limejaa ucha Mungu na kila mwanajumuiya hiya malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. “Hiki mnacho kifanya ni chema mmeacha shughuli zenu, waume zenu, watoto na marafiki badala ya kusherehekea nao sikukuu hii mmeona mje kutoa faraja kwa kuwatembelea hawa wagonjwa kwa kuw...