Posts

Showing posts from 2026

BAKWATA TABORA WAPONGEZWA KUANZISHA MRADI WA KITEGA UCHUMI

Image
  BAKWATA TABORA WAPONGEZWA KUANZISHA MRADI WA KITEGA UCHUMI Na Allan Kitwe, Tabora BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoani Tabora limepongezwa kwa kuanzisha mradi wa kitega uchumi wa jengo la ghorofa tano utakaochochea maendeleo ya Baraza hilo, waumini na jamii kwa ujumla. Pongezi hizo zimetolewa jana na Waziri wa Ujenzi Alhaj Abdallah Hamis Ulega alipokuwa akitoa salamu za Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye Maulid ya Kumbukumbu ya Mazazi ya Mtume Muhammad S.A.W mjini hapa.   Ameeleza kuwa Mheshimiwa Rais amewatakia kila la heri katika maulid hayo na ameomba waendelee kuombea amani na utulivu wa nchi ili vibaraka na wote wasioitakia mema nchi yetu wasipate nafasi. ‘Ndugu zangu nawaombeni tutumie hadhara hii kumwombea afya njema Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan na kuombea amani na utulivu wa nchi yetu, kwa kuwa mahali pasipo na amani na utulivu hakuna maendeleo’, ameeleza. Waziri Ulega amebainisha wazi kuwa BAKWATA Tabora wana dhamira ya dhati kuinua...

MWENYEKITI UVCCM KIBAHA, AWATAKA VIJANA KUSHIRIKI MICHEZO ILI KUEPUKA MAGONJWA.

Image
  MWENYEKITI UVCCM KIBAHA, AWATAKA VIJANA KUSHIRIKI MICHEZO ILI KUEPUKA MAGONJWA. Na mwandishi wetu , Kibaha Vijana wameaswa kuhakikisha wanakuwa na uzalendo na kutunza amani katika   nchi yao ikiwa pamoja na kuachana na tabia ya kukaa vijiweni na badala yake wajitokeze kwa wingi katika  kushiriki kikamilifu katika michezo mbali mbali lengo ikiwa ni kujenga afya na kuondoikana na magonjwa yasiyoambukizwa. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM) Wilaya ya Kibaha mjini Ramdhani Kazembe kwa alipokiuwa mgeni rasmi katika Bonanza la Tangini kwa niaba ya mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa wa Pwani  Alhaj Mussa Mansour.   Pia Kazembe amesema  kwamba Alhaj Mansour ameahidi kushirikiana bega kwa bega na viongozi wa Jogging zote za Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na kwamba atajipanga kukutana nao kwa ajili ya kuweka mikakati  madhubuti  ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kukibwa katika kusap...

VEDMA KUCHONGA BARABARA KIMANGE - PONGWE MNAZI

Image
  VEDMA KUCHONGA BARABARA KIMANGE - PONGWE MNAZI Na Omary Mngindo, Kimange KAMPUNI ya Vedma Investment imekabidhiwa Barabara kutoka Kimange mpaka Pongwe Mnazi, Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, iichonge ili ipitike vipindi vyote. Hayo yamebainishwa na Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) wilayani hapa kupitia Meneja Bupe Angetile, mbele  ya Diwani wa Kata Juma Gurumo akimtambulisha Mkandarasi huyo. Akizungumza kwenye kikao hicho, Meneja Bupe alisema kuwa wamepokea kiasi cha shilingi milioni 130, zitazojenga Kilometa 12 ambapo kati ya hizo zitatengenezwa 9 zilizosalia kilometa tatu ni zile korofi zitazopewa kipaumbele kikubwa. "Kwa kiasi tulichonacho tukisema tuweke changarawe yote haitotufikisha popote, tumeona tuweke kipaumbele maeneo korofi ikiwemo kwenye vilima ili tuondoe changamoto zinazotokea kipindi cha mvua," alisema Mhandisi Bupe. Kwa upande wake Diwani Gurumo alianza kumpongeza Meneja huyo kwa kuweza kumkabidhi Mkandarasi ...

WAZIRI AWESO ATOA WIKI MBILI MRADI WA MAJI NACHINGWEA KUANZA KUTOA HUDUMA

Image
  WAZIRI AWESO ATOA WIKI MBILI MRADI WA MAJI NACHINGWEA KUANZA KUTOA HUDUMA NA HADIJA OMARY  LINDI. Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso, amemuagiza mkandarasi wa kampuni ya Emirates Builders Company Ltd kuhakikisha ndani ya wiki mbili mradi wa Uboreshaji wa Huduma ya Maji katika Mji wa Nachingwea unaanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi. Gharama za Mradi huo ni shillingi bilioni 2, 587,672,026.00 na unaotakiwa kihudumia watu wapatao 45,000 wa wilaya hiyo ya Nachigwea ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 90 Waziri Aweso ametoa agizo hilo wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa katika Kijiji cha Mkumba, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha wananchi wa Nachingwea wanaanza kunufaika na huduma hiyo kwa wakati. Agizo hilo la Waziri Aweso limetolewa mara baada ya Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mhe. Fadhili Liwaka, kulalamikia uhaba wa maji safi na salama jimboni humo na kuiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto hiyo. Mbunge Liwaka...

KATIBU NEC ATAKA WENYE ULEMAVU KUCHANGAMKIA MIKOPO

Image
  KATIBU NEC ATAKA WENYE ULEMAVU KUCHANGAMKIA MIKOPO Na Allan Kitwe, Tabora   KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Rabia Hamid amewataka Vijana na Makundi mengine ya kijamii yenye ulemavu kuchangamkia mikopo inayotolewa na serikali ili kujikwamua kiuchumi. Ametoa wito huo jana alipokuwa akiongea na wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Chama na Serikali, makundi ya kijamii na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ukumbi wa Chuo cha Tabora Polytechnic. Ameeleza kuwa fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi zinazotolewa na serikali ya CCM chini ya Mwenyekiti wake Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hazibagui mtu. ‘Nimetembea maeneo mbalimbali na kushuhudia vikundi vya vijana, akinamama na watu wenye ulemavu vikinufaika na mikopo nafuu isiyo na riba ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri pasipo ubaguzi wowote, hii ni fursa’, ameeleza. Rabia amesisitiza kuwa watu wenye ulemavu wanaweza, h...

WAKULIMA WA TUMBAKU TABORA WALILIA BEI NZURI

Image
  WAKULIMA WA TUMBAKU TABORA WALILIA BEI NZURI  Na Allan Kitwe, Tabora WAKULIMA wa zao la tumbaku Mkoani Tabora wameeleza kusikitishwa na Makampuni yanayonunua zao hilo kujiamulia bei wanayotaka wenyewe wakati wa masoko jambo ambalo hupelekea mkulima kupata hasara kubwa. Hayo yamebainishwa kwenye kikao cha siku moja cha Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku (WETCU) kilichofanyika jana katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Themi Hill mjini hapa. Ismail Ramadhan , mkulima kutoka chama cha msingi Mwibiti, Wilayani Sikonge ameeleza kuwa katika msimu uliopita asilimia 80 ya tumbaku yao yote ilinunuliwa kwa bei ya dola 1.2 kwa kilo tofauti na bei elekezi ya dola 1.95. ‘Makampuni mengi yanatunyonya sana, haiwezekani bei elekezi ya soko kwa kilo ni dola 1.95 halafu mnunuzi aje kununua kwa bei anayotaka mwenyewe, hili haliingii akilini, huu ni wizi, tunaomba serikali itusaidie kuwadhibiti,’ ameeleza. Gelard Kusaya, mkulima kutoka Wilaya ya Uyui, amela...

MKUU WA MKOA ARUSHA AKUTANA NA WENYE HOTELI NA WADAU WA UTALII

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Septemba 24, 2026 amekutana na kuzungumza na Wamiliki wa Kampuni za Utalii, wamiliki wa Hoteli, Waongoza watalii, wamiliki wa kumbi za burudani, wapagazi na wasanii wa Mkoa wa Arusha, akiwataka kutumia vyema fursa za ujio wa Bunge la dunia (IPU) linalotarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 05, 2026 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC). "Wabunge wa IPU watakuwa zaidi ya 2, 500 na kila Mbunge ana msaidizi wake na wengine watakuja na familia na wapo wanaopanga kwenda kutalii, sasa hii ni fursa na nimeona niwaambie ili mchangamkie fursa hii, watu hao watalala kwenye hoteli zetu, watakula kwenye migahawa yetu, watataka kwenda kuona vivutio na zaidi watu hawa wakija wanaangalia pia vitu vingine kama uwekezaji, biashara na kupanga kurudi tena- Wakichagua huduma yako hakikisha unawaachia tabasamu warudi tena kwako na niwaombe Tanzania inajulikana kwa amani na ukarimu na sisi tukatoe taswira hiyo wakati wa kutoa huduma ...

KILOSA YAANZA MAANDALIZI YA KUKABILIANA NA EL NINO - DC SHAKA APIGA MARUFUKU MAFUNZO, AAGIZA FEDHA ZINUNUE VIFAA VYA DHARULA

Image
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Shaka Hamdu Shaka ameongoza Kikao Maalum cha Kamati ya Maafa ya Wilaya kilichojumuisha Kamati ya Ulinzi na Usalama na wadau mbalimbali kujadili maandalizi ya kukabiliana na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Akifungua kikao hicho, Mhe. Shaka amesema Wilaya ya Kilosa imejifunza kutokana na athari za mafuriko ya miaka ya nyuma na safari hii maandalizi yote yatajikita kwenye vitendo, sio kwenye makaratasi. Amefafanua kuwa uamuzi huo ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyeagiza mikoa na wilaya zote kuchukua tahadhari mapema na kuhakikisha taarifa za TMA hazibaki kwenye makaratasi bali zinafuatwa na hatua za vitendo. Akizungumza kwa msisitizo, DC Shaka alisema: _"Wilaya ya Kilosa tumeamua fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya maafa zitanunua vifaa vya dharura vinavyoonekana. Sitaki kusikia mafunzo, semina na w...

MWANRI AWAPA SOMO MAKADA WALIONOLEWA.

Image
  MWANRI AWAPA SOMO MAKADA WALIONOLEWA. Na Omary Mngindo, Kibaha NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Aggrey Mwanri amewataka washiriki wa Mafunzo ya Makada wa vyama vya kisiasa kwenda kuyatumia vizuri. Mwanri ametoa Rai hiyo katika kufunga Mafunzo ya siku 45 ya uongozi kwenye shule ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoa wa Pwani, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Msumbiji (FRELIMO), Chakil Aboobacar. "Mafunzo haya yanaashiria mwanzo wa kukiandaa kizazi kijacho cha Makada na viongozi wa vyama dada kutoka nchi zetu, niwaombe mkawe mabalozi wazuri wa kuyaeleza mliyojifunza," alisema Mwanri. Alipongeza kuwa, "Mmepata nafasi ya kujifunza masuala yanayohusu maendeleo ya nchi zetu, Wakufunzi wamenyakai kubwa sasa ni wajibu wenu kwenda kwenye vyama vyeu mkaunganishe vyama vyenu, Serikali na Wananchi,"alisema Naibu Katibu huyo. Mkuu wa Shule hiyo Prof. Marcelina Chijoriga alisema kuwa mafunzo yalitaraji kuwa na washiriki 60 ikiwa ni walengwa ...

TITF YAANDAA TAMASHA LA SANAA ZA UFUNDI ARUSHA

Image
  TITF YAANDAA TAMASHA LA SANAA ZA UFUNDI ARUSHA Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Tanzania International Tourism Festival (TITF) imeandaa tamasha la Sanaa za ufundi litalalofanyika kuanzia tarehe 6 hadi 11 Oktoba jijini Arusha. Tamasha hilo linalenga kuunganisha Sanaa, Ufundi, Utamaduni, Utalii na Uchumi wa Ubunifu, pamoja na kutoa fursa za masoko, biashara na uwekezaji kwa wazalishaji wa bidhaa za Sanaa na ufundi. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Edward Buganga alisema TITF imezishirikisha BASATA, Bodi ya Filamu Tanzania na COSOTA katika maeneo yanayohusiana na majukumu yao. Alisema tamasha hilo litafanyika katika Viwanja vya General Tyre, Njiro, Arusha. Alisema BASATA itashiriki katika maeneo yanayohusu maendeleo na ukuzaji wa sanaa, wasanii na wadau wa sanaa, pamoja na kuhamasisha fursa zinazotokana na uchumi wa ubunifu. Buganga alisema Bodi ya Filamu Tanzania itashiriki katika maeneo yanayohusu tasnia ya filamu na ...

VIJANA MANISPAA TABORA WALAMBA MKOPO WA MIL 109

Image
  VIJANA MANISPAA TABORA WALAMBA MKOPO WA MIL 109 Na Allan Kitwe, Tabora HALMASHAURI ya manispaa Tabora imewezesha Kikundi cha Vijana cha Umoja mkopo usio na riba wa shilingi milioni 109 ambao umewasaidia kununua gari aina ya Fuso Figher 16 ili kufanya mradi wa kusafirisha madini ya ujenzi. Mradi huo umeleta neema kubwa kwa vijana hao kwani tangu wamepata gari hilo kila siku wana uhakika wa kuingiza kiasi cha shilingi laki 5 au zaidi kutokana na usafirishaji wa madini ya ujenzi. Akizindua mradi huo leo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Wazo Michael Mwang’onda amepongeza ubunifu wa vijana hao wa kuanzisha mradi ambao utawaingiza kipato halali na cha uhakika. Aidha amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dk John Pima na Madiwani kwa kusimamia vizuri utoaji mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili kuwainua kiuchumi. Amesisitiza kuwa mikopo hiyo ni utekelezaji agizo la serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia...

RAIS WA ZANZIBAR ATOA POLE KUFUATIA KIFO CHA MAMA FATMA KARUME.

Image
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa salamu za pole kwa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Amani Abeid Karume, pamoja na familia, ndugu na jamaa, kufuatia kifo cha Mama Fatma Karume, aliyekuwa mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, kilichotokea leo, tarehe 21 Septemba 2026. Rais Dkt. Mwinyi amesema amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa, akieleza kuwa anaungana na familia ya Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki cha majonzi. Amesema Marehemu Mama Fatma Karume amekuwa sehemu muhimu ya historia ya Zanzibar na Tanzania, akiwa mwenza wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar. Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu amsamehe na amrehemu Marehemu Mama Fatma Karume na amjaalie makaazi mema Peponi, pamoja na kuipa familia subira katika kipindi hiki kigumu.

GREEN ACRES YAANZA KUFUNDISHA AKILI MNEMBA

Image
  GREEN ACRES YAANZA KUFUNDISHA AKILI MNEMBA Na Mwandishi Wetu Mkururugenzi wa shule ya Green Acres ya Mbezi Beach Salasala jijini Dar es Salaam, Jacklline Rushaigo ameelezea namna shule hiyo ilivyoanza  kufundisha Teknojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA  ili kwenda sanjari na ulimwengu kidijitali. Akizungumza kwenye mahafali ya darasa la saba na shule ya awali ambapo wanafunzi 60 walihitimu elimu ya msingi, Jackline alisema Shule hiyo inatambua umuhimu wa kuzingatia teknolojia za kisasa katika ufundishaji. “Tumeongeza ubora na ufanisi kwenye TEHAMA, wanafunzi wetu wanajifunaza masuala ya akili mnemba wakiwa wadogo hapa shuleni na mambo yanayoendana na uhalisia wa utanzania wetu na dunia ya sasa,” alisema “Tunawapa taaluma ambayo hata wakiwa nje ya shule wanaweza kufanya vitu mbalimbali vya kujiajiri na kujiingzia kipato, Green Acres tunataka mwanafunzi akimaliza hapa awe na ujuzi wa kutosha kabisa kumwezesha kufanya mambo makubwa,” alisema Aliwataka wahitimu wa darasa l...