Siku moja
tu baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe John Pombe Joseph Magufuli kutangaza kuwa Serikali itanunua korosho kwa Bei
Tshs 3300/= kwa kilo moja na Zoezi kusimamia Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) huku akipiga Marufuku Uingizwaji
wa korosho kimagendo kutoka nje ya Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Newala, Mhe Aziza Mangosongo amemkamata Mtu
Mmoja akiingiza Korosho kimagendo Magunia zaidi 90 yenye kilo zaidi 100
kila moja katika Maeneo ya Mpakani akivusha korosho Wakati wa Operation Maalumu
inayoendelea Wilayani humo.
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama, Wilaya ya Newala, Mhe Aziza Mangosongo akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Wilaya hiyo Pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Newala katika
Operesheni Hiyo.
“Mhe Aziza ametoa wito kwa wananchi waendelee kutoa
Ushirikiano kwa Serikali kuendelea kufichua Vitendo Vichafu kutaka kuihujumu
nchi na Ukiukwaji wa Sheria.”
No comments:
Post a Comment