Amana Bank leo Tarehe 18,
Novemba 2018 imeshirikiana na wananchi wa eneo la Mbagala kufanya usafi wa
mazingira ikiwa ni sehemu ya kuwa pamoja na wateja wao.
Pamoja na kufanya usafi
huo wa mazingira uliowashirikisha wananchi mbalimbali wa eneo hilo wakiongozwa
na Umoja wa Madereva wa Kusini mwa Tanzania (UMAKUTA) Benki hiyo pia ilikabidhi
vifaa vya kufanyia usafi na kuhifadhia taka kwa UMAKUTA.
Akizungumza mara baada ya
kumaliza kufanya usafi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dkt. Muhsin
Salim Masoud amesema Amana Bank ni
kawaida yao
kujitolea katika shughuli mbalimbali za kijamii.
Alisema wameamua kufanya
usafi huo wa mazingira kama utangulizi wa
kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo inaanza rasmi kesho Tarehe 18
Novemba 2018.
Aliongeza kuwa, katika
wiki ya huduma kwa wateja ambayo inakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka
saba sasa toka Benki hiyo ianze kutoa huduma za kibenki Tarehe 24 Novemba 2011.
Aliongeza kwa kusema kuwa,
Amana Bank ambayo ni Benki pekee inayofuata misingi ya sheria za kiislamu hapa
nchini na kutoa huduma bora za kibenki kwa watu wote, inathamini umuhimu wa
usafi wa mazingira katika juhudi za kujenga jamii bora.
Aidha, alitumia nafasi
hiyo kuwashukuru wateja wake na jamii kwa ujumla kwakuwa pamoja toka Benki hiyo
ilipoanza kutoa huduma hapa nchini.
Amewaomba wateja wa Amana
Bank na watanzania kwa ujumla kutembelea katika matawi ya Benki hiyo katika
kipindi hiki cha huduma kwa wateja ili waweze kujipatia huduma mbalimbali za
kibenki ikiwemo zawadi mbalimbali, fursa ya kuhudumiwa na Mkurugenzi mtendaji,
mameneja wakuu na wakuu wa idara
mbalimbali katika Benki hiyo.
Dkt. Muhsin, alisema Amana
Bank katika kuhakikisha inawapatia wateja wake huduma bora za kibenki imekuja
na huduma mpya ya mikopo kwa vikundi ambapo wakopaji watakopa bila ya kuwa na
dhamana kwani dhamana itakuwa kikundi chao weneyewe.
Katika wiki ya huduma kwa
wateja, Dkt. Muhsin alisema wateja watapata punguzo maalum la bei ya viwanja
vinavyotolewa kwa njia ya mkpo usiokuwa na riba kupitia Amana Bank kwa kushirikiana
na Property International Ltd. (PIL) ambao watakuwepo katika matawi yote ya Dar es Salaam ili kuonesha
viwanja vilivyopo katika miradi malimbali.
Kwa upande wake Katibu
Mtendaji wa Umoja wa Madereva wa Mabasi ya Kusini mwa Tanzania, (UMAKUTA) Yusuf
Malabe ameishukuru Benki hiyo kwa kushiriki zoezi la usafi katika eneo hilo na kuwakabidhi vifaa
vya kufanyia usafi.
Malabe alisema Amana Banki
ni Benki ya kwanza kuonyesha mfano huo toka walipoanza shughuli zao katika
kituo hicho mabasi Mbagala.
Alisema kwa kitendo
walichokifanya Amana Bank ni wazi kuwa Benki hiyo inawajali wateja wake na
jamii kwa ujumla hivyo wana kila sababu ya kuwaunga mkono kwa kufungua Akaunti
katika Beniki hiyo.
Amana Bank imekabidhi
Vifaa vya kufanyia usafi katika eneo la kituo cha mabasi Mbagala ambavyo ni
Ndoo za kuhidhia taka 20, Reki za kukusanyia taka, Fagio na Buti zitakazovaliwa
wakati wa kufanya usafi.
Katika zoezi hilo la usafi
huduma za kibenki zilikuwa zikiendelea ambapo watu mbalimbali waliweza kufungua
Akaunti zao, kuuliza maswali na kupewa miongozo kuhusu mikopo ya aina zote
inayotolewa na Amana Bank bila ya riba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dkt. Muhsin Salim Masoud, akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza zoezi la usafi kituo cha mabasi Mbagala leo Novemba 18, 2018.
Wafanyakazi wa Amana Bank, wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kumaliza shughuli ya kufanya usafi wa mazingira kituo cha mabasi Mbagala leo Novemba 18, 2018.
Wafanyakazi wa Amana Bank
wakiwa pamoja na wakazi wa Mbagala wakijiandaa kufanya usafi mapema asubui ya
leo Novemba 18, 2018.
Meneja Mkuu wa Biashara wa Amana Bank, Dasu Musa (kulia) akiwa na Meneja wa Tawi la Tandamti, Juma Yamlinga wakiendelea na ukaguzi wa maeneo waliyosafisha kuona kama kuna uchafu umebaki.
Usafi
ukiendelea katika eneo la Mbagala
Meneja Mkuu wa Biashara wa Amana Bank, Dasu Musa (kulia) akiwa na Meneja wa Tawi la Tandamti, Juma Yamlinga wakiendelea na ukaguzi wa maeneo waliyosafisha kuona kama kuna uchafu umebaki.
Meneja Mkuu wa Biashara wa
Amana Bank, Dasu Musa, akibadilishana mawazo na Meneja wa Masoko wa Benki hiyo, Jamali Issaeneo la Mbagala mara baada ya kumaliza kufanya usafi eneo la Mbagala.
Umoja wa Madereva wa Mabasi ya Kusini mwa Tanzania, (UMAKUTA) wakiwa na vifaa vya kufanyia usafi walivyokabidhiwa na Amana Bank leo Novemba 18, 2018.
Pamoja na usafi
uliofanyika eneo la Mbagala, wafanyakazi wa Amana Bank waliweza kuendelea na
majukumu yao ya kuwahudumia wateja hapo hapo kama wanavyoonekana wakiwafungulia Akaunti wateja wapya.
No comments:
Post a Comment