Kikundi cha Pwani generation queens walipotembelea kituo cha Afya Chalinze kutoa msaada wa vifaa vya kinamama waliojifungua.
.......................................................
NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
WODI ya uzazi katika kituo cha
afya Chalinze,mkoani Pwani inakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwepo ufinyu
wa jengo hali inayosababisha wakati mwingine akinamama wazazi kusongamana na
kulazimika kulala wawili katika kitanda kimoja.
Aidha kina tatizo jingine la upungufu
wa vitanda na watumishi wa afya hasa madaktari .
Akikabidhiwa msaada wa vifaa vya
akinamama waliojifungua kutoka kwa kikundi cha Pwani generation queens
,mganga mfawidhi wa kituo hicho Salama Masukuzi alisema kuwepo
kwa mlundikano wa wagonjwa kunatokana na upungufu wa majengo ya wodi ya
uzazi pamoja na vitanda .
Alieleza ,kwasasa wapo maafisa
tabibu wanne ,madaktari wasaidizi wawili na daktari mmoja ambao bado ni
wachache kutekeleza majukumu yao ya kutoa huduma bora ya kiafya .
“Kituo hiki kinapokea wagonjwa
mbalimbali na wengine wakitokea kwenye zahanati 44 zinazozunguka halmashauri ya
Chalinze suala ambalo linawawia vigumu kutekeleza wajibu wao ” alifafanua
Salama .
Alieleza wamepata manesi wanne
kupitia ajira mpya, ameishukuru serikali lakini aliiomba kuwaboreshea
zaidi huduma ya afya ili kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wa akinamama wa
Chalinze,akiwemo Demertia Milichadesi pamoja na Mariam Muhoja walisema
wanapata shida katika kununua drip,vifaa vya uzazi na kipimo cha kujua wingi wa
damu ambacho hutakiwa kwenda nje wakati mjamzito akiwa tayari yupo wodini.
“Tumekuwa tukipata shida ya ukosefu
wa vifaa kwa ajili ya kujifungulia na wakati mwingine inatubidi kwenda
dukani kununua na uwezo wetu kifedha ni mdogo ,tunqshindwa kumudu
gharama za matibabu”
Demertia aliwashukuru Pwani
generation queens kwa misaada waliyoipata na kuomba wadau na vikundi vingine
vikumbuke kusaidia kituo cha afya Chalinze.
Akikabidhi msaada wa vifaa mbali
mbali katika wodi ya uzazi kwenye kituo hicho cha afya , Mwenyekiti wa kikundi
cha Pwani Generation Queens Betty Msimbe alisema wamesaidia kutokana na
kubaini kuwepo kwa upungufu wa vifaa hasa kwa wanawake wajawazito
ambao wanakwenda kupatiwa matibabu na kujifungua.
Betty alieleza,wapo wanawake ambao
wamekuwa wakipata shida pindi wanapokwenda katika zahanati, vituo vya
afya na hospitali kwa ajili ya kujifungua hivyo wakaona kuna umuhimu wa kutoa
msaada huo.
No comments:
Post a Comment