Wednesday, June 10, 2020

Waziri wa nishati ataka wawekezaji kuzalisha vifaa vya kusafirisha gesi hapa nchini





Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ametoa wito kwa wadau wa viwanda kutengeneza Vifaa vya kusafirisha nishati ya mafuta na gesi hapa nchini dhamira ikiwa ni kuharakisha mchako wa kuanza miradi ya usambazaji lakini pia kupunguza gharama za uzalshaji.

Alisema uhitaji wa mabomba kwa miradi inayoendelea bado ni mkubwa na kwamba hadi sasa mahitaji ya mabomba ya gesi ni kilometa  zisizopungua 2,250 na mita za luku ni 8,000 hadi 10,000 kwa mwaka .

Aidha akizungumzia kasi ya usambazaji wa mabomba ya gesi majumbani, Kalemani alisema kuna mafanikio makubwa yamepatikana ikiwamo usambazaji huo kuongezeka kutoka Kaya 70 hadi kufikia Kaya 1000 kwa Miaka mitatu.

Aliongeza kusema kuwa kuagiza vifaa nje ya nchi kunapoteza mapato ya nchi, agizo alilolitoa linalenga kulinda mapato, uzalishaji wa mabomba koki ,vyuma, nyaya utasaidia  kujenga uchumi wa nchi kupitia sekta ya viwanda ,"Dkt.Kalemani .

Faida ya kuzalisha mabomba nchini itasaidia kuongezeka kwa kasi ya kusambaza gesi na hivyo kuwapa nishati wananchi kwa wakati.

Naye Naibu Waziri wa  Wizara hiyo Stephen Byabato   amesema serikali inaendelea kutekeleza ilani ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuendelea kuwaunganisha nishati ya umeme mjini na vijijini.

Alisema Rais Dkt.Magufuli anaamini vijana wana uwezo kiutendaji ndio maana amemteua kumsaidia kutekeleza majukumu ya Wizara hiyo chini ya Waziri Dkt.Kalemani.

Awali akizungumza kwenye Mkutano huo, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo la Petroli TPDC Dkt. James Mataragio amesema wanaendelea na ujenzi wa vituo vitano vya kujaza gesi asilia kwenye magari katika mkoa wa dar es salaam huku kukiwa na mpango wa kupeleka nishati hiyo jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel Ateta Na Madereva Wa Malori, Namanga

 
Arusha.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amefanya ziara katika mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga Jijini Arusha na kuzungumza na madereva wa malori yanayokwenda Kenya ili kusikiliza changamoto zinazowakumba.

Dkt. Mollel amefanya ziara hiyo leo, ikiwa ni sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakumba madereva hao, katika kipindi hiki ambacho Dunia imekumbwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Dkt. Mollel amesema kuwa, Serikali imeliona tatizo hilo na kuweka wazi kuwa itaongeza kasi katika kuhakikisha inapata suluhu ya changamoto wanazokumbana nazo madereva hao katika eneo la mpaka wa Namanga.

“Nimekuja kuwaambia poleni, lakini Serikali yetu itaenda kwa kasi ya ajabu kuhakikisha kwamba hili tatizo lenu katika mpaka huu linatatuliwa ” alisema.

Aidha, Dkt. Mollel amewataka madereva hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho, Serikali inatafuta utatuzi wa changamoto yao, huku akiwapa salamu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli na kusema anawapenda sana.

Mbali na hayo Dkt. Mollel alisema kuwa changamoto hii iliyojitokeza katika mpaka wa Namanga ni suala mtambuka ambalo linahusisha Wizara zaidi ya moja, huku akiweka wazi kuwa suala hili lina uhusiano wa kibiashara na uchumi baina ya nchi hizo.

Nae, dereva wa malori yanayokwenda nchini Kenya Bw. Abdullah Hassan amesema kuwa, kama madereva hawakubaliani na majibu ya vipimo wanavyopewa kutoka Kenya kutokana na vipimo hivyo kuonesha idadi kubwa ya madereva kuwa na ugonjwa wa Corona jambo ambalo sio kweli.

“Tunaishi maisha magumu sana kutokana na hali iliyojitokeza, na kunachosikitisha zaidi, sisi hatukubaliani na vipimo ambavyo tunapimwa upande wa pili.

Kwa upande wake, Japhet Jeremiah alisema kuwa, wamekuwa wakiombwa kiasi cha shilingi 2000 za Kenya ili kuandikiwa kuwa hawana Corona, hali aliyeweka wazi kuwa ni uonevu kwa madereva kutoka Tanzania.

“Sisi kero yetu, tumekuwa tukipima Kenya tumeambiwa tuna Corona, na mimi wiki mbili nilipima nikapewa cheti nina Corona lakini ukweli ni kwamba sina Corona na sijawai tumia dawa yoyote mpaka sasahivi” alisema

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA AFRIKA MASHARIKI KUANZA KARIBUNI




Na Iisac Thadeo

 Kampuni inayosimamia mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki  (EACOP)imefanya kikao na waziri wa Nishati nchini Tanzania Dr.Medard Kalemani kwa lengo la kuitaarifu Serikali maendeleo ya mradi katika eneo la Ziwa Albert nchini Uganda pamoja na maendeleo ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki  (EACOP)

Vilevile kampuni ya Total na wizara ya Nishati wamezungumzia mipango ya kuendelea na mazungumzo ya makubaliano ya Serikali husika (wenyeji)wa makubaliano ya wabia /wanahisa,pamoja na makubaliano ya maswala ya Usafirishaji ili kuleta uiano wa makubaliano yote kwa ajili ya kuendelea na maamuzi ya mwisho ya uwekezaji

Kwa upande wake waziri WA Nishati wa Tanzania na kwa niaba ya Serikali ya Tanzania amesema leo ni siku nzuri kwa wenzetu wa Total wametuarifu wamekamilisha majadiliano Kati Yao na Sino kutoka Uingereza na Total wamechukua his a asilimia 67 na nyingine zilizobaki za SINO kwa maana hiyo atakuwa ni mwekezaji mkubwa.

Aidha waziri Kalemani alisema amewaomba Total na kuwataka yote wanayosema wayafanye kwa haraka

Mkutano huo ulifanyika zilipo Ofisi ndogo za wizara ya Nishati jijini Dar es salaam na kuudhuliwa na wadau mbalimbali wa Sekta hiyo kuwepo Katibu mkuu wa wizara hiyo mheshimiwa Zena

Saturday, May 23, 2020

KAMATI YA ALAT PWANI YAIFAGILIA MIRADI YA UJENZI WA SOKO NA MACHINJIO KIBAHA MJI.

No description available.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika kiwanda cha viuwadudu vya mbu walipofanya ziara katika halmashauri ya mji Kibaha kwa ajili ya kutembnelea na kugagua miradi mbali mbali ya maendeleo.(Picha na Victor Masangu)
 ..........................................

VICTOR MASANGU, PWANI.
 
KAMATI ya jumuiya ya umoja wa serikali za mitaa (ALAT Mkoa wa Pwani imewaagiza watendaji na watumishi wa halmashauri kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa  kuweka mipango madhubuti ambayo itasaidia  kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa muda uliopangwa bila ya kucheleweshwa kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Hayo yalibainishwa  na Mwenyekiti wa Alat Mkoa wa Pwani  Hatibu Chaulembo wakati wa ziara ya kutembelea miradi mitatu ya kimikakati ikiwemo ujenzi wa machinjio ya kisasa, ujenzi wa soko, pamoja na kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuulia mazalia ya mbu  viuwadudu ilivyopo katika halmashauri ya Mji Kibaha na kuongeza kuwa wameridhishwa na hatua ambayo imefikia.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema kwamba serikali ya awamu ya tano imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo hivyo inatakiwa isimamiwe ipasavyo na kukamilika kwa wakati ili kuweza kuwasaidia wanannchi wa maeneo mbali mbali katika Mkoa wa Pwani waweze kupata fursa za ajira na wengine kujiajiri wao wenyewe.

“Sisi kama kamati ya Alat Mkoa wa Pwani tumefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi mitatu ya kimikakati katika halmashauri ya mji Kibaha ikiwemo Soko kubwa la kisasa, ijenzi wa machinjio ya kisasa pamoja na kujionea shughuli mbalin mbali za uzalishaji amabzo zinafanyika katika kiwanda cha viuadudu hivyo kwa pamoja tumerudhishwa na mwenendo mzima japo kuna mambo mengine yanatkiwa yafanyiwe kaza zaidi,”alisema Chaurembo.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Musa Gama ambaye pia ni Katibu wa Alat Mkoa wa Pwani alimshukuru Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbali mbali ambayo itaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.

Gama alibainisha kuwa utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ni njia moja wapo ya kuwaondolea wananchi wimbi la umasikini hivyo juhudi ambazo zinafanywa na serikali ya awamu tano chini ya usimamizi mzuri waRais Dk. John Pombe Magufuli hivyo kumamilika kwa miradi hiyo kutakuwa ni chachu kubwa katika kukuza uchumi wa nchi.

“Mimi kama Katibu wa Alat Mkoa wa Pwani naweza kusema nimejifunz amambo mbali mbali katika ziara hii amabyo tumeifanya katika halmashauri ya mji wa Kibaha kwani nimeweza kujionea ujenzi wa machinjio makubwa ya kisasa pamoja na soko jipya ambayo hivi vyote kwa pamoja vitaweza kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi pindi vitakapokuja kukamilika kw ahiyo ni hatua kubwa sana ambayo imefanyika,”alisema Gama.

Nao baadhi ya wajumbe wa kamati YA Alat Mkoa wa Pwani akiwemo Hamisi Dipakutile, Mshamu Munde pamoja na Jenipher Omolo alisema kwamba serikali ya awamu ya tano imeweza kufanya mambo mengi katika sekta mbali mbali hivyo wana imani kuwa katika siku za usoni miradi hiyo pindi ikikamilika italeta maendeleo makubwa kwa wananchi.
No description available.
Baadhi ya wajumbe wa kamati  ya jumuiya ya umoja wa serikali za mitaa ALAT Mkoa wa Pwani wakiwa wanapata maelekezo ya namna ya  kutengeneza dawa ambayo inauwa mazalia ya mbu katika kiwanda cha viuatilifu kilichopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani. walipofanya ziara ya siku moja kwa ajili ya kujionea  shughuli mbali mbali za miradi ya maendeleo (Picha na Victor Masangu)
 No description available.
Wajumbe wakiwa katika maabara ya kuchanagnyia dawa wakifuatilia maelekezo kwa umakini kutoka kwa mtaalamu wa madawa hayupo pichani walipotembelea kiwanda cha viuadudu vya mbu kilichopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani .(Picha na Victor Masangu)
No description available.
Mwonekano wa  baadhi ya wajumbe wa kamati ya Alat Mkoa wa Pwani wakiwa katika chumba amabcho kuna mitambo maalumu ambayo imetengenezwa kwa ajili ya kuchanganyia madawa ya aina mbali mbali ikiwemo dawa kwa ajili ya kuulia mazalia ya Mbu.(Picha na Victor Masangu)
No description available.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ambaye pia ni Katibu wa kamati ya Alat Mkoa wa Pwani Musa Gama akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa wataalamu wa kuchanganya madawa kwa ajili ya kuulia mbu katika kiwanda cha viuadudu walipofanya ziara kwa ajili ya kujionea shughuli mbali mbali.(Picha na Victor Masangu)
No description available.
Baadhi wa wajumbe wa kamati ya Alat Mkoa wa Pwani wakiwa kwa nje ya soko la kisasa ambalo linajengwa Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo.(Picha na Victor Masangu)
No description available.
Mmoja w awajumbe wa kamati ya Alat Mkoa wa Pwani akiwa katika chumba chenye mitambo ambayo inatumika katika utengenezaji na uzalishaji wa madawa ya kuulia mazalia ya mbu. (Picha na Victor Masangu)
No description available.
Katibu wa Alat Mkoa wa Pwani Musa Gama kati kati akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ziara ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo katika halmashauri ya Kibaha mji.(Picha na Victor Masangu)