ULEGA ATAKA VIKUNDI VYA BAGAMOYO VIKOPESHWE FEDHA ZA HALMASHAURI, KWA KUTUMIA VIZURI FURSA YA UCHUMI WA BLUU.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akizungumza na wana kikundi cha ufugaji wa Majongoo Bahari kilichopo Kaole kata ya Dunda Halmashauri ya Bagamoyo, kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge. ................................................ Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, kuvipatia fedha vikundi viwili vilivyopo Bagamoyo ambavyo vinajishughulisha na ufugaji wa Majongoo Bahari na kilimo cha Mwani. Ulega ametoa agizo hilo Tarehe 25 Februari 2022 alipotembelea vikundi hivyo ili kujionea shughuli zinazofanywa na vikundi hivyo. Naibu waziri huyo alifika Bagamoyo kufungua kikao kazi cha mkakati na kampeni ya kuhamasisha shughuli za ukuzaji viumbe Bahari ambacho kilijumuisha wataalamu kutoka mikoa ya Dar es salaam na Pwani lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya fursa zilizopo kwenye uchumi wa bluu ambao unjumuisha mazao ya Bahari ikiwemo ufugaji wa Majongoo Bahari, Ufugaji wa K...