DADA POWA, KAKA POWA, MARUFUKU BAGAMOYO.
Mkuu wa Wiaya ya Bagamoyo, Alhajj, Majid Mwanga amemuagiza Mkuu wa Polisi wilaya ya Bagamoyo, kuwakamata wale wote wanaojishughulisha na biashara ya ngono wanawake na mashoga, maarufu kama dada powa, na kaka powa, ili kukomesha vitendo hivyo katika Wilaya ya Bagamoyo. Mh. Majid, aliyasema hayo wakati wa kuzindua Mpango Mkakati juu ya Maambukizi ya VVU na UKIMWI wa Wiaya ya Bagamoyo uliozinduliwa jana Tarehe 28 Agosti 2017. katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Bagamoyo. Alisema katika mitaa ya Bagamoyo wapo kina dada powa na kaka powa, ambao ni kichocheo cha maambukizi ya VVU na UKIMWI na kwamba sasa ni marufuku kuona dada powa na kaka powa katika wilaya ya Bagamoyo. Aliongeza kwa kumtaka Mkuu wa Polisi wilaya ya Bagamoyo, kufanya doria katika mitaa ya Bagamoyo ambayo inafahamika kwa biashara ya ngono na kuwakamata wale wote wanaohusika lengo likiwa ni kupambana na maambukizi ya VVU na UKIMWI lakini pia ni kurudisha utamaduni wa Bagamoyo ambao ni kuwa na ...