Posts

Showing posts from February, 2018

VIONGOZI WALIOKULA FEDHA ZA WAKULIMA WA KOROSHO WARUDISHE.

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema viongozi wa Vyama vya Ushirika waliokula fedha za wakulima wa korosho wilayani Masasi wazirudishe na wakishindwa mali zao zikiwemo nyumba zitauzwa ili kufidia. Pia Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bw. Gelasius Byakanwa ahakikishe anawasaka viongozi wa chama Ushirika cha Msingi cha Nanyindwa wilayani Masasi ambao wamekula fedha za wakulima na kisha kutoroka. Amesema viongozi wa vyama vya Ushirika katika wilaya hiyo si waaminifu, ambapo mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya sh. bilioni 2.3 za wakulima ziliibiwa na viongozi hao, ambapo mwaka 2017/2018 sh. bilioni 1.7 zimeibiwa. Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo jana (Jumatatu, Februari 2018) alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi pamoja na watumishi wa wilaya akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara. Alisema viongozi wa Ushirika wa Nanyindwa ambao wametoroka ni Michael Mkali, Yusuph Mataula, ambapo alimuagiza Bw. Byakanwa kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo ...

WATOTO 6 WAWASHIWA VIFAA VYA USIKIVU (COCHLEAR IMPLANT).

Image
Mtaalam wa Huduma ya Usikivu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Mathayo Majogoro Alfred (katikati) akiunganisha kifaa cha usikivu cha nje na cha ndani ili mtoto Matilda Katobesi aweze kusikia kwa mara ya kwanza. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Pua, Koo na Masikio, Dkt. Edwin Liyombo akifuatilia na kushoto ni mama wa mtoto huyo, Angelina Cosmas. ................................ Watoto sita ambao wamewekewa vifaa vya usikivu Januari mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo wameanza kusikia kwa mara ya kwanza baada ya kuwashiwa vifaa hivyo.  Kuwashwa kwa vifaa hivyo kumeleta furaha kwa wazazi kwani wameshuhudia watoto wao wakisikia sauti kwa mara ya kwanza na hivyo kuwajengea matumaini ya watoto hao kuanza maisha mapya. Zoezi la kuwawashia vifaa hivyo (Switch On) limefanyika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  kwa kushirikiana na wataalaam kutoka Medel Austria ambao ndio wasambazaji wa vifaa hivyo. Akizungumza na waan...

NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA ASHUHUDIA UZINDUZI WA HUDUMA ZA KISASA KITUO CHA AFYA NYAMWAGA TARIME

Image
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiangalia vifaa vilivyopo katika kituo cha afya cha Nyamwaga kilichopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara.  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akitoa nasaha wakati alipokwenda kushuhudia uzinduzi wa huduma za kisasa katika kituo cha Afya cha Nyamwaga kilichopo Wilaya ya Tarime mkoa wa Mara. Baadhi ya wananchi wakisikiliza nasaha zilizokuwa zikitolewa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula wakati wa uzinduzi wa kituo cha afya cha Nyamwaga kilichopo Tarime mkoa wa Mara. Sehemu ya majengo ya kituo cha Afya cha Nyamwaga kilichopo Tarime mkoa wa Mara . PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI-WANMM

NMB YASAIDIA VIFAATIBA VYA MIL. 5, HOSPITALI YA BAGAMOYO.

Image
Meneja wa NMB kanda ya Mashariki, Aikasia Muro (wa nne kulia) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga (mwenye suti) moja ya vifaatiba walivyotoa msaada kwa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, wanaoshuhudia wa pili kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya bagamoyo, Ally Ally Issa na wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Hospitali ya Wilaya Bagamoyo, Mwajuma Saidi Masaiganah. ............................................... Benki ya NMB imesaidia vifaa tiba katika Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo vyenye thamani ya shilingi milioni tano. Akizungumza katika kukabidhi vifa hivyo, Meneja wa NMB kanda ya Mashariki, Aikasia Muro alisema Benki hiyo imefikia hatua hiyo ikiwa ni katika mipango yake ya kurudisha faida inayopata kwenye jamii. Alisema NMB katika mipango yake imekuwa ikishiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kusaidia katika sekta ya Elimu, kusaidia vifaa vya ujenzi, sekta ya Afya na kusaidia watu katika kipindi cha majanga kama ya mafur...

DC BAGAMOYO ATOA SIKU 3 WINDE (RAZABA)

Image
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga,kihutubia wakuu wa idara katika Ukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo Tarehe 23 February 2018. Na Athumani Shomari  ..................................... Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga, ametoa siku tatu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, kufuatilia taarifa za watu wanaogawana viwanja katika shamba linalomilikiwa na Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA) lililopo kijiji cha Winde kata ya Makulunge. Mkuu huyo wa wilaya alitoa agizo hilo Tarehe 22 Februry 2018 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo, kufuatia taarifa za kuwepo watu wanaogawana viwanja ndani ya shamba hilo bila ya kujali mipaka na umiliki halali walionao RAZABA. Alimtaka mkurugenzi kumpa taarifa za kitaalamu kuhusu mipaka ya RAZABA ili kubaini ukubwa wa eneo lililovamiwa na kuangalia hatua za kuchukua ili kunusuru eneo hilo ambalo lipo chini ya umiliki wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar . Alisema hatua za haraka zichukuliwe ili kusitisha zoezi li...

DAWASA KUONDOA TATIZO LA MAJI BAGAMOYO.

Image
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, (katikati) akiongoza Mkutano wa kujadili upatikanaji wa maji Bagamoyo pamoja na kuanzisha mfumo wa kusafirisha maji taka. ...........................................................  Wadau wa maji wilayani Bagamoyo wamekutana kujadili namna ya kuboresha miundombinu ya maji safi pamoja na kuandaa mpango mkakati wa kuanzisha namna kusafirisha maji taka ili mji wa Bagamoyo ubaki safi na salama. Mwenyekiti wa Mkutano huo, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga alisema kufuatia kukua kwa mji wa Bagamoyo ipo haja ya kujadili namna bora ya kusafirisha maji taka badala ya kuwa na maeneo yasiyo rasmi kwa utupaji wa taka. Alisema lengo la mkutano huo ni kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mradi wa maji taka ambao DAWASA tayari wameshafanyia upembezi yakinifu juu ya utekelezaji wa mradi huo. Akizungumza katika Mkutano huo, Mhandisi wa Miradi Chrisitian Gava alisema katika kipindi cha mwaka 2014 mpaka 2016 Mamlaka ya maji safi na m...

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AWASHA KITUO CHA UMEME MBAGALA.

Image
Naibu waziri wa nishati awasha umeme kituo cha Mbagala baada ya mradi huo kukamilika. Kufuatia kuwashwa kwa kituo hicho, Wananchi wa Mbagala ,Kigamboni ,Tandika na Mkuranga na Wenye Viwanda watapata Umeme wenye Nguvu na wenye uhakika ambao hautokatika. Naibu waziri wa Nishati, amewapongeza wananchi wakazi wa maeneo hayo Kwa kuwa na subira huku akiwapa pole kwa kero ya umeme ya muda Mrefu. Aidha, alisema amewashukuru Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo ya Kigamboni Dk Ndungulile na Mhe Mangungu na Wakuu wa Wilaya Kwa kufuatilia Jitahada za kuondosha Kero hiyo ya Upatikanaji wa Nishati ya Uhakika katika Maeneo hayo. Alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli imefanya juhudi kubwa kutekeleza mradi huo ili wananchi waondokane na kero hiyo. Alisema kufuatia ushirikiano alionao yeye pamoja na Waziri wa nishati Dk Medard Kalemani wameweza kufanikisha Miradi mbalimbali ya Nishati ya umeme hapa nchini hali inay...

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MAHAFALI YA 34 YA CHUO KIKUU HURIA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki matembezi ya mahafali ya 34 ya Chuko Kikuu Huria pamoja na Mkuu wa chuo hicho Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda (kulia) kuelekea kwenye uwanja wa Halmashauri ya  Bariadi kwenye sherehe za mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania. .............................................................. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewakumbusha wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kuwa Vyeti walivyotunukiwa  ni tuzo halali kwa juhudi na jitihada walizoonesha darasani. Makamu wa Rais aliyasema hayo wakati wa sherehe za mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri Bariadi mkoani Simiyu. Makamu wa Rais alisema “ Jamii inategemea mtaipatia tuzo ya utendaji bora na ufanisi katika fani zenu utakao akisi viwango vilivyoainishwa kwenye vyeti vyenu”. Makamu wa Rais aliupongeza uongozi wa chuo kwa jit...