Posts

Showing posts from March, 2018

MAGAZETI YA LEO TAREHE 22 MACHI 2018.

Image

NAIBU WAZIRI SHONZA AONGOZA KUAGA MWILI WA JOHN MPONDA BAGAMOYO.

Image
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa mwalimu John Mponda, ambae alikuwa Mkufunzi Msaidizi daraja la 2, Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Mwalimu Mponda Pia alikuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, ( Bagamoyo International Festival of Arts and Culture) .  Naibu Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akizungumza wakati wa kuaga mwili wa Mwalimu John Mponda wa TaSUBa. ................................................. Naibu Waziri Habari, Sanaa na Utamaduni Juliana Shonza amesema Wizara yake itamkumbuka Mwalimu John Mponda kwani alikuwa kiunganishi kizuri kati ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) na wizara yake katika kufanikisha mambo mbalimbali ya Sanaa hapa nchini. Naibu Waziri huyo aliyasema hayo leo tarehe 21 Machi 2018 wakati wa kuaga mwili wa mwalimu John Mponda shughuli...

MAFISA HABARI TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI.

Image
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus akizungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID). .............................................. MAAFISA Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kuacha kufungia katika makabati na makabrasha taarifa chanya za utekelezaji wa mikakati, miradi na programu mbalimbali za Serikali na badala yake watangaze mafanikio hayo kwa umma. Hayo yamesemwa jana (Jumanne Machi 20, 2018) Mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu mwongozo wa uandish...