Saturday, July 31, 2021

MHE. RAIS SAMIA APOKEA NDEGE MPYA AINA YA BOMBADIER DASH 8-Q400

 No description available. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria kupokea Ndege Mpya aina ya Bombadier DASH 8-Q400 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania na kukodishwa kwa  Shirika la Ndege la ATCL ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 30  Julai, 2021. Wa pili kushoto ni Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango na wa tatu kulia ni waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasalimia Wananchi waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kumuunga Mkono kwenye mapokezi ya Ndege Mpya aina ya Bombadier DASH 8-Q400 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania na kukodishwa kwa  Shirika la Ndege la ATCL ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 30  Julai, 2021.

 No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kupokea Ndege Mpya aina ya Bombadier DASH 8-Q400 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania na kukodishwa kwa  Shirika la Ndege la ATCL ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30  Julai, 2021. IKULU.

 

 

Friday, July 30, 2021

RC KUNENGE AONGOZA WAKAZI WA MKOA WA PWANI KUPATA CHANJO YA UVIKO 19

 May be an image of 3 people, people sitting and people standing

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, Mkuu wa Mkoa wa Pwani amepata chanjo ya UVIKO 19 leo Julai, 30 2021.

 

Akichanjwa chanjo hiyo katikà viwanja vya kituo cha Afya cha Mkoani, Kibaha Mjini kunenge amewaasa Wanachi wa Mkoa huo kuwa ugonjwa upo na kuwataka kuchukua tahadhari wakati wote, amewataka Kuvaa barako, kunawa mikono na kuepuka mikusanyiko isiyo lazima.

 

Amemshukuru Mhe Rais kwa kupata chanjo, "nimechanja kwa hiari yangu mwenyewe mpaka sasa najisikia vizuri sijaona shida yeyote"

 

 

"Wananchi waje wachanje kwa hiari yao tunachotafuta ni salama" tumepata chanjo kidogo tunaendelea kuratibu upatikanaji wa nyingi zaidi na tutaitoa bila usumbufu. "Chanjo hii kwa sasa itatolewa kwa makundi ya Kipaumbele alisema Kunenge.

May be an image of 1 person, child, sitting and outdoors