Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa bungeni Jijini Dodoma.
......................................
Na Shamimu Nyaki –WHUSM.
Katika kuimarisha usikivu wa Shirika
la Utangazaji Tanzania (TBC) Serikali imeendela kuweka mikakati mizuri ya
kuongeza usikivu wa shirika hilo hapa nchini kutegemea na upatikanaji wa fedha.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Jijini
Dodoma na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe
alipokuwa akijibu swali la mbunge Mhe. Zaynab Matitu Vulli (Viti Maalum)
aliyeuliza Ni chanagamoto zipi zinazopelekea TBC kutosikika katika baadhi ya
maeneo ya Pwani ambapo Mhe. Waziri alieleza kuwa katika Bajeti ya mwaka 2016/17
maeneo mengi ya nchi yaliongezewa usikivu.
“TBC ina mitambo ya kurushia
matangazo ya redio ya masafa ya FM katika Wilaya ya Kisarawe ambayo
hufikisha matangazo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani katika
masafa ya 87.8 MHz kwa idhaa ya TBC Taifa, 90.0 MHzkwa idhaa ya TBC FM na
95.3 kwa idhaa ya TBC International”.Alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha ameongeza kuwa katika Bajeti ya
mwaka 2016/17 TBC ilitekeleza mradi wa upanuzi wa usikivu katika Wilaya tano
zilizopo mpakani ambazo ni Wilaya za Longido, Rombo,Tarime,Nyasa na Kibondo.
Vilevile katika Bajeti ya mwaka
2017/18 mradi wa usikivu katika mkoa wa Mtwara na Wilaya ya Lushoto mkoani
Tanga ulitekelezwa ambapo hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu TBC ilikua na vituo
thelathini na tatu vya kurushia matangazo katika masafa ya FM kwenye Wilaya 102
kati ya 161 nchi nzima.
Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa Serikali
inaendelea kuhakikisha kuwa TBC inapanua usikivu ambapo kwa mwaka huu wa fedha
maeneo ya Unguja na Pemba,Simiyu,Njombe,Songwe,Lindi maeneo ya Nangurukuru
pamoja na Mkoa wa Morogoro maeneo ya Morogoro Vijijini,Bondwa na Mahenge
yatafikiwa.
No comments:
Post a Comment