Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani
leo (Novemba 12.2018) amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijiji
REA kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wake.
Waziri Kalemani amewaambia waandishi
wa habari leo jijini hapa kuwa bodi hiyo iliundwa mwaka 2017 kwa mujibu
wa sheria ya wakala vijijini No.8 ya mwaka 2005.
“Kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu 9 (3)(b) cha sheria No. 8 ya nishati vijijini ya 2005 nimeamua kuivunja bodi kwa kutengua uteuzi wa mwenyejuti pamoja na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya wakala wa nishati vijijini kuanzia leo tarehe 12 novemba 2018″amesema Kalemani.
Aidha amesema kuwa bodi nyingine
itaundwa baadae kwa mujibu wa sheria ya nishati vijijini ya mwaka 2005 Bodi
hiyo iliyokuwa ikiongozwa na mwenyekiti wake Gigion Kaunda ilidumu kwa muda wa
mwaka mmoja baada ya mwaka jana.
Dk, Kalemani amesema kuwa Bodi mpya
itaundwa badaye kwa mujibu wa sheria ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005.
Wajumbe wa Bodi ambao wametenguliwa
ni pamoja na Mhandisi Innoceent Lwogwa,Happiness Mhina,Stella Mandago,
Scholastica Jullu,Amina Chinja,Teobard Sabi na Michael Nyagoga.
No comments:
Post a Comment