Naweed Mulla mwenye kofia
ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Highland
Estate akimuonyesha mbunge wa chalinze jinsi mkonge unavyofanyiwa hatua mpaka
kufikia mwisho kwa kusafirishwa.
...................................................
Na Shushu
Joel,chalinze.
SERIKALI
imeombwa kutoa elimu kwa wananchi wote nchini ili waweze kulima zao la mkonge
kama wanavyolima mazao mengine ya biashara kwa manufaa yao katika
kujiongezea kipato.
Rai hiyo
imetolewa na Naweed Mulla mkurugenzi wa kampuni ya Highland Estates
Limited inayojishughulisha na ulimaji wa na uuzaji wa zao la mkonge, iliyoko
katika halmashauri ya chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani alipokuwa
akizungumza na mbunge wa jimbo hilo mara baada ya kutembelea kiwandani hapo.
Alisema kuwa
endapo wananchi watahamasika kulima mkonge hapa nchini basi zao hili litazidi
kupanda thamani na kuongeza tija kubwa katika kilimo cha mazao ya
biashara na hata kuachana na kulima mazao mengine kutokana na zao hilo kuwa
katika nafasi za juu hapa duniani.
“Zao
la mkonge ni utajiri uliojifichaambao wananchi wa tanzania asilimia kubwa
hawajatambua thamani ya zao hilo ila kwa haraka haraka ni zao lenye mafanikio
ya haraka kwa wakulima “Alisema Mulla
Aliongeza
kuwa kama serikali ikitoa elimu kwa wakulima na kutilia mantiki kwa wakulima
kila mmoja kulima angalau ekali 3 za mwanzo ili waweze kuona manufaa yake hivyo
watanzania watalima mkonge kwa wingi.
Naye ....ni
moja ya wafanyakazi katika kiwanda hicho anaeleza kuwa kiwanda hicho
kimekuwa msaada mkubwa kwa wao na wananchi walio karibu na eneo hilo katika
nyanja mbalimbali ya kijamii.
Aliongeza
kuwa sitahiki zote zinazohitajika kwa watumishi zinatolewa na kiwanda hicho ila
tu kulingana na kiwango chako cha elimu na uzoefu katika nafasi hiyo.
Kwa upande
wake mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete alisema kuwa kuna haja ya
serikali kuhamasisha zao hili nchini ili kuwanufaisha wakulima wadogo wadogo
kutokana na hali halisi ya uhitajikaji wake kuwa mkubwa katika nchi
zilizoendelea.
Aliongeza
kuwa kiwanda hicho cha Mkonge kinahitaji mikonge ya kutosha hivyo wananchi
wakilima zao hilo litawasaidia katika kujipatia kipata na kuweza kufanya
maendeleo mengine.
Aidha mbunge
huyo amempongeza mkurugenzi wa kampuni hiyo kwa jinsi anavyowajali watumishi
wake kwa kuwapatia mahitaji sitahiki na kwa wakati kwani hakuna llamiko
alilopewa kuhusu unyanyasaji kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho.
“Nimetembelea
kiwanda hicho ili kujionea uzalishaji wa zao la mkonge na hatua zake za
upatikanaji wake nimejifunza vitu vingi lakini kikubwa ni kuwahamasisha
wananchi kulima zao la mkonge kitu ambacho kitawafanya wakulima kujiongezea
kipato” Alisema Ridhiwani.
Pia
ameipongeza kampuni hiyo kwa jinsi inavyijitolea katika ufanikishaji wa miradi
ya kimaendeleo kwa wananchi walio jirani na kiwanda hicho kwa kuwajengea
zahanati,majengo mawili ya madarasa na mambo mengine mengi kwa kusudi la
kuwasaidia walio kwenye mazingira ya karibu.
Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa na mkurugenzi wa kampuni ya Highland Estate Limited Naweed Mulla wakiangalia mkonge ulioanikwa.
Mbunge Ridhiwani
akiangalia hatua za mwisho za zao la mkonge mara baada ya hatua zote kufanyika
hapo sasa tayari kwa kusafirishwa kwenda nje kwa ajili ya mauzo.
No comments:
Post a Comment