Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) kama mnavyofahamu linashiriki Ulinzi wa
Amani ndani na nje ya Bara la Afrika.
JWTZ linasikitika kuwataarifu kwamba limewapoteza wapiganaji
wake watatu (3) waliofariki kwa tarehe tofauti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (DRC) na Afrika ya Kati (CAR) wakiwa kwenye jukumu la Ulinzi wa Amani
baada ya kushambuliwa na vikundi vinavyosadikiwa kuwa ni vya waasi.
Mashujaa wetu waliouwawa ni Koplo Mohamed Mussa, Koplo Erick
Masauri John na Praiveti Musa Shija Machibya. Miili ya marehemu hao
tayari imepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na
kuhifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.
Heshima za mwisho kwa mashujaa wetu hao zitatolewa katika
sehemu ya kuagia Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kesho tarehe 23 Novemba 2018
kuanzia saa 2.30 asubuhi. Vyombo vya Habari na Wananchi wanakaribishwa
tuungane katika kuaga mashujaa wetu.
Mungu azilaze Roho za Mashujaa wetu mahali pema Peponi, Amina.
No comments:
Post a Comment