Posts

Showing posts from December, 2017

KOROSHO ZAINGIZA BILIONI 39 PWANI

Image
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga. MKOA wa Pwani ,tayari umeuza tani 19,815 ambazo zimeingiza  zaidi ya bilioni 39 tofauti na msimu uliopita ambapo uliuza tani 13,000 na kupata bilioni 33.## Mkoa huo umejiwekea lengo la kuuza tani 25,000 hadi 30,000 kwa msimu huu ambao  minada yake ya korosho ikiwa bado inaendelea . Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,aliyasema hayo Mkuranga ,wakati akizungumzia changamoto na mafanikio waliyoyapata msimu wa korosho 2017/2018 . Alieleza ,mbali ya hayo wakulima wa korosho mkoani Pwani wakiwa bado wanadai zaidi ya bilioni tano. Mhandisi Ndikilo alisema ,kuuza tani 19,815 hadi sasa ni mwanzo mzuri wa kufikia malengo yao waliyojiwekea msimu huu. Alisema ,hatua hiyo imetokana na serikali kutoa pembejeo bure katika msimu huu na mfumo wa stakabadhi ghalani. Alibainisha ,licha ya mafanikio hayo lakini kuna changamoto zimejitokeza tangu kuanza kwa minada mwaka huu ikiwemo uhaba wa magunia . Kero nyingine...

CGP. DKT. JUMA MALEWA AHUTUBIA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA 2017.

Image
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza Baraza Maalum la kufunga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018. Baraza hilo limehudhuriwa na Maafisa na Askari kutoka vituo mbalimbali vya Magereza Mkoani Mbeya, Chuo cha Magereza Kiwira na Chuo cha Ufundi Mbeya ambapo Baraza hilo limefanyika leo Desemba 31, 2017 katika Viwanja  vya Magereza Mkoani Mbeya. Baadhi ya Askari wa kike wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali vya Magereza ya Mkoa wa Mbeya wakisikiliza hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(hayupo pichani) katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018. Wakuu wa Magereza yaliyopo Mkoani Mbeya wakifuatilia kwa umakini mkubwa maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza aliyoyatoa katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018. Mkuu wa Magereza Mkoani Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kijida Mwakingi akitoa taarifa fupi ya Mkoa wak...