Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akikata utepe ikiwa ni kuashiria uwashwaji wa
umeme katika kijiji cha Igula, Wilaya ya Iringa Vijijini.
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akibonyesha kitufe cha kuwashita taa na kingora
ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa kazi ya kuwasha umeme katika kijiji cha
Igula, Wilaya ya Iringa Vijijini. Kijiji cha Igula ni moja ya vijiji
vinavyonufaika na mradi wa kupeleka kwenye vijiji vilivyopitiwa na Njia kuu ya
Umeme KV 400.
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu kabla ya kuzungumza na wananchi na kuwasha
umeme katika kijiji cha Igula iliyopo halmashauri ya Iringa Vijijini. Kutoka
kushoto ni Katibu tawala, Hashimu Komba na Diwani wa Kata ya Kihologota,
Paziyano Kayage.
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wanafunzi wa darasa la sita wa
Shule ya Msingi Ikengeza iliyopo halmashauri ya Iringa vijijini. Shule hiyo ni
miongoni mwa taasisi ambazo zimenufaika na mradi wa kupeleka umeme kwenye
vijiji vilivyopitiwa na Njia kuu ya Umeme ya KV 400(BTIP-VEI).
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akimbana msimamizi wa Kampuni ya Sengerema
Engineering Group, Bryson Chengula baada ya kutolidhishwa na kazi ya
utekelezaji wa miradi ya REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza ambao unatarajia
kufikia tamati Juni 30 mwakani.
No comments:
Post a Comment