Posts

Showing posts from October, 2017

RAIS. DKT. MAGUFULI AFUNGUA VIWANDA VIWILI JIJINI MWANZA.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha madawa cha  Prince Pharmaceuticals kilichopo Buhongwa nje kidogo jijini Mwanza. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage mara baada ya kufungua kiwanda cha Victoria molders and polybags kilichopo Igogo jijini Mwanza. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mafundi wa Kiwanda cha Victoria molders and polybags mara baada ya kutengeneza Tanki la kuhifadhia maji.

MADIWANI KISARAWE WAMFUKUZA KAZI MGANGA MFAWIDHI WA ZAHANATI

Image
BAADHI ya madiwani wa wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani ,wakionekana kusikiliza jambo  wakati wa baraza la madiwani lililofanyika mjini hapo . Picha na Mwamvua Mwinyi ......................................   Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe BARAZA la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani, imeazimia kumfukuza kazi mganga mfawidhi wa zahanati ya Mtakayo wilayani humo Dkt. Emmanuel Benedict. Benedict amefukuzwa katika nafasi hiyo kutokana na kutowajibika ipasavyo,utoro na kufunga zahanati kwa siku tisa hali iliyokwamisha utoaji huduma ndani ya siku hizo . Mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe Hamisi Dikupatile akizungumza baada ya kumalizika kwa baraza la madiwani alieleza wamechukua hatua hiyo kufuatia mtumishi huyo kufanya uzembe. Alisema maamuzi hayo yamefanyika kwa mujibu wa kanuni za utumishi ya mwaka 2003 jedwali A ,kifungu namba 42 ambapo kuna mapendekezo ya adhabu ikiwemo kushushwa cheo,kupunguziwa mshahara au kufukuzwa kazi . ...