Mwenyekiti wa Jumuiya ya
waislamu iliyopo Mkoani Wilayani Kibaha Alhaji Mussa Sekule akizungumza na
waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kumalizika kwa sherehe za
maadhimisho ya miaka 10 ya jumuiya hiyoo.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
...................................................................
VICTOR MASANGU,
KIBAHA
KATIKA kuunga mkono juhudi
za serikali ya awamu ya tano katika kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo
kupitia sekta ya kilimo Jumuiya ya Waislamu iliyopo eneo la Mkoani kata ya
Tumbi Wilayani Kibaha imeweka mipango madhubuti ya kupambana na wimbi la
umasikini na kujikwamua kiuchumi kupitia mradi maalumu ambao
utakuwa unajikita zaidi katika shughuli mbali mbali za kilimo cha
mazao ya biashara pamoja na chakula.
Hayo yamebainishwa na
Katibu mkuu mstaafu wa Jumuiya hiyo ya waislamu Mkoani Omari Hatibu
wakati wa sherehe za kilelel cha maadhimisho ya miaka 10
ambayo yamefanyika katika msikiti wa Wipazi uliopo mjini Kibaha na
kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa dini pamoja na serikali.
Aidha Katibu huyo
alibainisha kwamba pia Jumuiya yao kwa sasa ina mipango mingine
mbali mbali ikiwemo kufanya jitihada kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa
chuo maalumu ambacho kitaweza kuwapa fursa waumini wa kiislamu
kujifunza mambo mbali mbali ya uongozi ikiwemo masuala ya kuwa wazalendo
na nchi yao pamoja na kudumisha amani na upendo kupitia masomo ya kidini
watakayofundishwa.
“Kwanza kabisa tunapenda
kumshukuru Mungu kwa jumuiya yetu hii kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake
ni hii kwetu sisi ni hatua kubwa zaidi na kitu kikubwa ni kuendelea kuisaidia
jamii katika mambo mbali mbali katika sekta ya elimu, afya, maji pamoja na
makundi ambayo yanamahitaji maalumu,”alisema Hatibu.
Naye Mwenyekiti wa jumuiya
ya waislamu mkoani iliyopo Wilayani Kibaha Alhaji Mussa Sekule amesema
kwamba kwa kipindi chote cha miaka kumi wameweza kuisaidia jamii katika
Nyanja mbali mbali ikiwemo sekta ya elimu, afya, pamoja na kuvisaidia vituo vya
watoto yatima na watu wenye mahitaji maalumu.
Kwa upande wake mmoja wa
waumini walioshiriki katika maadhimisho hayo Haji Saleh ambaye pia ni
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Wipaz ambayo inajihusisha na masuala mbali
mbali ya kijamii amewaasa waislamu na wananchi wote kwa ujumla
kuhakikisha wanaungana kwa pamoja kwa ajili ya kudumisha hali ya amani na
upendo na washirikiane kikamilifu katika kuleta mabadiliko chanya
ya kimaendeleo.
Pia alisema kuwa suala la
kuwepo kwa amani na upendo ni jambo ambalo linaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa
kuwepo kwa ushirikiano wa hali na mali kutoka kwa serikali pamoja na
wananchi wenyewe kuweza kupata fursa ya kushiliki kikamilifu katika
masuala ya msingi hususana katika miradi ya maendeleo.
Baadhi ya viongozi wa
Jumuiya ya waislamu Mkoani wakijadiliana jambo wakati wa kilele cha sherehe
za maadhimisho hayo ya kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake. (PICHA NA
VICTOR MASANGU)
Mmoja wa waumini wa
kiislamu Haji Saleh ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Wipaz
akizungumza jambo na waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari wakati wa
maadhimisho hayo ya jumuiya ya waislamu Mkoani yaliyofanyika katika msikiti wa
Wipaz mjini Kibaha. (PICHA NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment