Naibu waziri wa nishati
,Subira Mgalu, ambae ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Pwani akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Chalinze.
..........................................................
NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE.
MWELEKEO wa mradi wa
wakala wa umeme vijiji (REA III )mzunguko wa pili unatarajia kuanza June 2019
,ili kuvifikia vijiji ambavyo vimesalia katika utekelezaji wa mradi huo awamu
ya kwanza.
Aidha mradi wa ujazilizi
unatarajiwa kuanza mwezi machi mwakani huku mradi wa peri -urban utakaohusisha
mkoa wa Pwani na Dar es salaam
unategemewa kupata mkandarasi Januari mwaka huo na umeshatengewa sh.bilioni
83.
Naibu waziri wa nishati
,Subira Mgalu alieleza hayo katika kikao cha madiwani cha kata kwa kata
kilichofanyika Lugoba Chalinze, mkoani Pwani ,wakati akitolea ufafanuzi
utekelezaji unavyoendelea wa miradi ya umeme vijijini na mipango ya miradi hiyo
ya kimkakati .
Alisema,kwa jitihada zote
hizo za serikali kutekeleza miradi ya vijijini tayari vijiji 4,702
vimeshafikiwa hadi sasa .
Subira alisema maeneo yote
iliyolengwa wakandarasi wanaendelea na kazi .
Kwa mujibu wake ,mkoa wa
Pwani katika REA awamu ya III vipo vijiji 150 ,ambapo baadhi ya vijiji
vimeshawekwa miundombinu na vingine mita .
Alilielekeza shirika la
umeme (TANESCO) kuendelea kusambaza umeme kwenye maeneo ya wananchi pasipo
kusubiri utekelezaji wa mradi wa REA.
“Serikali inafanya kazi
,nia yetu ni ushindi na sio ushindi tuu katika chaguzi zinazokuja bali tuwe na
majibu ya namna tunavyotekeleza ilani vijijini na vitongojini” alisisitiza
Subira.
Nae mwenyekiti wa
halmashauri ya Chalinze ,Saidi Zikatimu aliiomba serikali kuwa, vijiji
vinavyopitiwa na umeme vifikie vitongoji vyake na kufikia vijiji ambavyo tangu
dunia iumbwe havina umeme.
Diwani wa kata ya Miono
,Juma Mpwimbwi alieleza bado kuna tatizo la ukosefu wa umeme kijiji cha
Mkwajuni na Makaomakuu ambapo tangu wapimiwe nguzo hawajapelekewa vifaa wala
kuandaa miundombinu .
No comments:
Post a Comment