Posts

Showing posts from June, 2024

ETDCO YAENDELEA KUJENGA MIUNDO MBINU YA KUSAFIRISHA UMEME MRADI WA TABORA - KATAVI 132kV

Image
  Kaimu Meneja Mkuu Kampuni ya ETDCO CPA Sadock Mugendi, Amesema Wanaendelea kujenga miundo mbinu ya Umeme Nchini ikiwemo Njia ya kusafirisha umeme kutoka  Tabora  hadi Katavi ambao ni mradi wa kusafirisha  Umeme na tayari  Mradi Umefkia Asilimia 67. Mugendi amesema ETDCO ni kampuni Tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania na ni suluhisho la miundo mbinu ya umeme kwani ipo kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundo mbinu ya kusafirisha na kusambaza umeme. Kaimu Meneja Mkuu CPA Sadock Amesema Mradi wa Kutoka Tabora kwenda Katavi wenye Urefu wa kilometa 383 wa msongo wa 132kV ambao Unatarajiwa kumalizika Mwaka huu kupelekea    Mkoa wa Katavi kupata  Umeme wa Uhakika pia Kuipunguzia Gharama Tanesco za Kununua Mafuta ya Dizeli kwajili ya Jenereta ili kuzalisha Umeme kwenye Mkoa Wa Katavi. CPA Sadock Ameipongeza Serikali kuendelea kuwekeza kwenye Sekta ya Nishati ili Kuhudumia Wananchi wake vizuri, Amesema Hayo Wakati Akitembelea Mradi wa Kimkakati wa Tabora ...

KIKWETE MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE WA SADC YUKO LESOTHO

Image
  NA MWANDISHI WETU, LESOTHO Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo tarehe 26 Juni, 2024, yuko katika Ufalme wa Lesotho kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Jopo la Wazee wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Jopo hili la Wazee wa SADC ambalo Makamu Mwenyekiti wake Mheshimiwa Paramasivum Pillay B. Vyapoory, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Mauritius, limekutana na Serikali na wadau mbalimbali ndani ya Ufalme wa Lesotho, kama mwendelezo wa juhudi ya kusaidia upatikanaji wa utulivu wa kisiasa katika Ufalme huo.  Jopo limekutana na Mhe. Ntsokoane Samuel Matekane, Waziri Mkuu wa Ufalme wa Lesotho; Mhe. Nthomeng Justina Majara, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Sheria na Masuala ya Bunge; Mhe. Mamonaheng Mokitimi, Mwenyekiti wa Seneti; Viongozi wa Vyama vya Upinzani; Mhe. Constance Seoposengwe, Balozi wa Afrika Kusini nchini Lesotho na wadau mbalimbali.

WAZIRI MKUU AZINDUA VITABU VYA HISTORIA YA BUNGE

Image
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua vitabu vya historia ya Bunge ambavyo vitasaidia kuhamasisha tafiti na kujua zaidi kuhusu mchango wa Bunge katika maendeleo ya jamii nchini. Amesema kuwa vitabu hivyo pia vitakuwa kielelezo cha mafanikio na changamoto ilizopitia Bunge la Tanzania katika kudumisha demokrasia na utawala wa sheria. “Historia yetu ni sehemu ya mchango wetu kwa jumuiya ya kimataifa katika kukuza amani, utulivu na maendeleo.” Amesema hayo leo (Jumatano, Juni 26, 2024) wakati wa uzinduzi wa vitabu viwili vya historia ya bunge katika ukumbi wa Pius Msekwa, Jijini Dodoma.Vitabu vilivyozinduliwa ni Kitabu cha Historia ya Bunge kutoka 1926-2024 na Wabunge wa Tanzania na nafasi zao kuanzia mwaka 1965-2023 “Kumbukumbu za historia ya Bunge zinaweza kuchochea utafiti wa kitaaluma na maendeleo ya nadharia za kisiasa na utawala. Watafiti wanaweza kutumia taarifa hizi kujenga ufahamu mpya na kupendekeza mifumo bora ya kisiasa.” Kwa upande wake Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson a...

TANESCO, WAWEKEZAJI BINAFSI LUDEWA WAFIKIA MAKUBALIANO

Image
  TANESCO, WAWEKEZAJI BINAFSI LUDEWA WAFIKIA MAKUBALIANO Ni kuhusu TANESCO kukabidhiwa  miundombinu ya kusambaza umeme* Ludewa kujengwa kituo cha Kupokea na Kupoza umeme Kapinga asema Vijiji 70  kati ya  76 Mbulu vimepatiwa umeme Imeelezwa kuwa, Serikali na Wawekezaji wanaowauzia umeme wananchi katika baadhi ya kata za Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wamefikia makubaliano ya kisheria ili miundombinu ya usambazaji umeme katika Kata hizo ikabidhiwe kwa Shirika la Umeme Tanzania  (TANESCO). Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga leo Juni 26, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu maswali mbalimbali ya Waheshimiwa Wabunge akiwemo Mbunge wa Ludewa, Mhe. Zacharius Kamonga aliyetaka kufahamu Serikali itamaliza lini changamoto za bei na mgao wa umeme katika Kata hizo. Kapinga ameongeza kuwa, hatua zote za makabidhiano zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Mwezi Julai, 2024 na baada ya kukamilika, TANESCO watabadilisha mita za umeme ili ziendane ...

CTI YALIA NA UTITIRI WA TOZO MIKOANI

Image
  Na Mwandishi Wetu   SHIRIKISHO la Wenye Viwanda (CTI), limeseme kuwepo kwa utitiri wa tozo katika kila mkoa na halmashauri kumekuwa kikwazo katika ustawi wa biashara na uwekezaji nchini.   Hayo yalisemwa  jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Shirikisho hilo, Leodegar Tenga katika warsha maalumu ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya viwanda vya chakula na vinywaji kupitia utafiti uliofanywa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utawala Bora na Maendeleo ya Wajasiriamali, Dk. Donath Olomi.   Utafiti huo ulioangazia namna tozo hizo zilivyo kikwazo kwa wafanyabiashara kwenye maeneo mbalimbali nchini.   Tenga alisema Dk Olomi ni mtafiti msomi na ameainisha vitu vingi ikiwemo mapendekezo ya kufuata kuondoa vikwazo hivyo, akisisitiza kuwa lengo ni kuwapa nafasi nzuri wafanyabiashara wakubwa wanaotamani kuja kuwekeza nchini.   Tenga alisema athari ya utofauti wa tozo unaathari kibiashara ikiwamo kuongezeka kwa bei za bidhaa, na hivyo kusababisha  mlaji kununua b...

CTI YASEMA BAJETI ITASISIMUA UKUAJI WA VIWANDA

Image
 Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Wenye Viwanda nchini (CTI), limepongeza bajeti kuu ya serikali kwa kuweka mambo muhimu ambayo yatachochea ukuaji wa viwanda nchini.   Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa shirikisho hilo, Leodegar Tenga, wakati akizungumza na waandishi wa habari.   Amesema serikali imekuwa sikivu kwa wenye viwanda na kila wanapokuwa na jambo wamekuwa wakifunguliwa milango ya majadiliano na kwamba hakuna jambo la wenye viwanda ambalo linakwama.   Amesema wenye viwanda wamefurahia sana bajeti ya serikali kwa kuzingatia uendelezaji wa miradi ya kimkakati kama reli ya kisasa SGR ambayo alisema itasiadia kwa kiwango kikubwa kukuza viwanda vya  ndani kuzalisha kwa wingi bidhaa.   Amesema miradi kama SGR inasaidia kukuza uchumi kwani viwanda vitazalisha kwa wingi na bidhaa kusafirishwa kwa urahisi tofauti na sasa ambapo usafirishaji umekuwa ukisababisha bei kupanda.   “Nchi ambayo iko makini inaendeleza miradi mikubwa kama ...

DKT. MPANGO AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA TAASISI YA KIMATAIFA YA UWEKEZAJI YA UINGEREZA.

Image
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Uingereza (BII) Nick O’Donohoe na ujumbe wake, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu, Dodoma.   Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuendelea kuwekeza nchini tangu mwaka 1949 katika sekta muhimu na za kipaumbele kwa uchumi wa Taifa ikiwemo Nishati, Kilimo na Chakula, Misitu, Huduma za Fedha, Huduma za Mawasiliano pamoja na kushirikiana na Benki za Tanzania ikiwemo Benki ya NMB.   Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeweka mkazo katika kuendelea kufungua uchumi kwa kufanya mageuzi muhimu yanayochochea na kuvutia biashara na uwekezaji. Ameongeza kwamba Serikali imeendelea kufanya mageuzi ya kisera kwa kuhakikisha sera na sheria zinazotabirika. Aidha, Serikali inaendelea kufanya mageuzi ya kitaasisi ili kuhakikisha ma...

RC LINDI AZIAGIZA HALMASHAURI KUANZISHA NA KUHUWISHA MADAWATI YA ULINZI MASHULENI

Image
  NA HADIJA OMARY, LINDI. Mkuu wa Mkoa wa Lindi ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa huo kuhakikisha zinafufua au kuunda madawati ya ulinzi ya watoto  sambamba na kuunda klabu za watoto mashuleni zitakazowasaidia kuelezea na kutatua changamoto zao Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kimkoa huko katika kijiji cha chienjele halmashauri ya Ruangwa Jana Juny 16/2024 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi , Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Patrick Sawale  amesema vyombo hivyo ni  muhimu  kwa ajili ya kutetea maslahi yao pindi watoto wanapokuwa wamefanyiwa ukatili.  Amesema ili Taifa liweze kuendelea kupiga hatua ni muhimu kutilia maanani mahitaji  ya watoto  ikiwa pamoja na watoto  masikini , walemavu na walio na mazingira magumu zaidi kutengewa mafungu toka katika bajeti kuu ya serikali na zile za Halmashauri. hata hivyo ameendelea  kuikumbusha Jamii kuwa inawajibu wa  kutoa taarifa na ushahidi kuhusu mtoto ambae...

SERIKALI YAENDELEZA JITAHADA ZA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA TEMBO

Image
  NA HADIJA OMARY, LINDI. Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na utalii imeendelea kujenga vituo  kupeleka asikari wa wanyama pori pamoja na vitendea kazi Katika maeneo yote yenye changamoto ya wanyama wakali na waharibifu aina ya Tembo ili kukabiliana na changamoto hiyo Hayo yameelezwa na Mratibu wa Mradi wa kutatua changamoto ya migongano baina ya binaadamu na Wanyama pori unaotekelezwa Katika wiliya za Liwale Mkoani Lindi, Namtumbo na Tunduru Mkoani Ruvuma Bw.Gideon Mseja alipokuwa anafungua mafunzo ya siku moja kwa waadishi wa vyombo mbalimbali vya habari yaliyofanyika huko Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma Mafunzo hayo yamewakutananisha waandishi 10 kutoka Katika Maeneo ya utekelezaji wa Mradi maafisa habari wa halmashauri , wawakilishi kutoka kitengo cha  mawasiliano wizara ya maliasili na utalii pamoja na maafisa Wa Serikali  Amesema changamoto hiyo ya wanyama wakali na waharibifu imeathiri Katika wilaya 44 ambapo Serikali imeendelea kuchukua Hatua mbalimbali Ka...

WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO KWA WATUMISHI WA UMMA

Image
  Awataka waondoe urasimu na kutowasumbua wananchi wanaowahudumia   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini kote wawatumikie wananchi ipasavyo na wahakikishe wanaondoa urasimu kwa kutowasumbua wananchi wanaokuja kupata huduma za kiserikali katika ofisi zao. “Epukeni tabia ya kuomba na kupokea rushwa, rushwa inaharibu maendeleo. Tusitumie maneno magumu kwa wananchi wetu maana eneo hili bado ni changamoto, tunalishughulikia au bado tupo kwenye mchakato, tunafanya tathmini, upembuzi yakinifu, tumieni lugha rahisi.“ Pia, Waziri Mkuu amewataka watumishi hao wazingatie taaluma zao na watoe ushauri kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma, wafike sehemu ya kazi kwa muda uliopangwa na watumie muda huo kufanya kazi za Serikali na waepuke kuwa na migongano ya maslahi katika kutekeleza majukumu na kusimamia rasilimali za umma. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Juni 12, 2024) kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Taasisi ya Maboresho ya Serikali ...

RAIS DK.MWINYI AISHUKURU TAASISI YA AL MAZRUI

Image
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Taasisi ya Al Mazrui Charitable Organisation ya Abu Dhabi kwa kuendelea kutoa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo afya , elimu na maji. Pia ameishukuru taasisi hiyo  kwa kutoa jengo lao kwa Serikali ilitumie kwa huduma za afya. Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo akizungumza na vijana wa Chuo cha ufundi Mubarak AL Mazrui  na alipotembelea eneo hilo Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe :11 Juni 2024. Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali imetoa kibali cha kuajiri vijana waliokuwa wanajitolea katika mashirika mbalimbali ya Serikali ikiwemo Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA).

MOTO WATEKETEZA BWENI BUKOBA

Image
  Na Alodia Babara, Bukoba, Bweni la wavulana katika shule ya sekondari Mugeza Mseto iliyopo kata ya Kahororo manispaa ya Bukoba mkoani Kagera limeteketea kwa moto na mali zote zilizokuwemo kuungulia humo chanzo cha moto huo bado hakijajulikana. Kaimu kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Kagera George Mrutu akizungumzia tukio hilo Juni 05, mwaka huu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, limetokea Juni 04, mwaka huu saa 8:15 usiku wakati wanafunzi wakiwa darasani wanajisomea. Mrutu amesema kuwa, jeshi hilo lilipokea taarifa kupitia simu yao ya 114 kutoka kwa mkuu wa shule juu ya kuwepo tukio la moto katika shule hiyo ndipo kikosi cha zimamoto kilielekea eneo la tukio walifika na kukuta moto ukiwa umeshasambaa kwenye bweni zima na kuanza juhudi za kuuzima. “Baada ya kufika tulikuta moto umeshasambaa bweni zima miali ya moto ikiwa inatokea madirishani moto umeshashika kwenye paa tulifanya juhudi za kuuzima moto huo ili usiendelee kuleta madhara, hatukuwe...

RUNALI YAWAJENGEA WAKULIMA  KITUO CHA MALIPO RUANGWA 

Image
  NA HADIJA OMARY, LINDI. HATIMAYE ucheleweshwaji wa Fedha za malipo ya wakulima wa Wilaya ya Ruangwa wanaohudumiwa na chama kikuu cha Ushirika Runali kinachojumuisha wakulima wa Wilaya za Ruangwa, Liwale na Nachingwea mkoani Lindi, itabaki historia baada ya chama hicho kujenga kituo cha malipo kitakachotumika kuandaa na kuhakiki malipo ya wakulima hao kwa haraka zaidi. Kituo hicho cha malipo kimejengwa katika Kata ya Lipande  Wilayani Ruangwa ambapo kimewekwa jiwe la msingi na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack  na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali Wilayani humo pamoja na viongozi wa vyama vya Msingi, Amcos za Mkoa wa Lindi. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Katibu Tawala wa Mkoa huo (RAS) Zuwena Omary baada ya kukagua jengo hilo na kuweka jiwe la msingi amekipongeza chama hicho kwa namna kinavyoendelea kuwekeza na kutoa huduma bora kwa wanachama wake kwa kuzikabili changamoto wanazokutana nazo. Pamoja na pongezi hizo  pia aliutaka u...