Posts

Showing posts from November, 2018

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ASHIRIKI MKUTANO MKUU WA 20 WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI ARUSHA.NOVEMBA 30,2018

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) .Novemba 30,2018(PICHA NA IKULU) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museven kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) .Novemba 30,2018

MALALAMIKO 74 UKATILI WA KIJINSIA YARIPOTIWA LINDI.

Image
NA HADIJA OMARY, LINDI Jumla ya Malalamiko (74) yanayohusu vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, mkoani humo,yamefikishwa katika Dawati sheria ,huku vitendo vya ubakaji vikiwa vinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa,mwaka 2017 Hayo yameelezwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa hiyo, Anna Maro alipokuwa anazungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG  Ofisini kwake mjini humo, kuhusiana na siku (16) kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika manispaa hiyo Maro alisema vitendo hivyo vimeripotiwa kituo cha Polisi cha Lindi mjini,kupitia Dawati lake la kijinsia, na kwamba wamefanyiwa ukatili huo,kipindi cha mwaka mmoja uliopita,kuanzia mwezi Januari hadi Disemba 2017. Alieleza kwamba vitendo vya ubakaji ndio unaoongoza kwa kuwa na Idadi kubwa (39),ikifuatiwa kujeruhi na Shambulio la mwili,iliyo na idadi (9) kila moja,Mimba za wanafunzi (7),kulawiti (3),wakati kutelekeza familia na matumizi ya Lugha za matusi ...

BABA MZAZI AUWA WATOTO WAKE WATATU BAGAMOYO.

Image
Kamanda wa polisi wa mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo . (picha na Mwamvua Mwinyi) ………………………. NA MWAMVUA MWINYI,PWANI JESHI la polisi mkoani Pwani ,limethibitisha kutokea kwa vifo vya watoto watatu akiwemo wa miezi kumi ,waliouawa kwa kunyweshwa sumu na baba yao mzazi. Chanzo cha kutenda kitendo hicho cha kikatili kinadaiwa ni kutokana na ugomvi mkubwa kati ya wazazi wa watoto hao. Kamanda wa polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa alieleza tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana huko kata ya Kibindu, Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo. Aliwataja watoto hao kuwa ni pamoja na Shaila Salehe miaka sita ,Nurdin Salehe (4)na Sabrat Salehe mwenye miezi kumi waliouawa kwa kunyweshwa sumu ambayo ni dawa ya kuulia magugu iitwayo Twiga Amine na baba yao mzazi Salehe Masokola (22),mkazi wa kijiji ...

MAKUSANYO HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAONGEZEKA.

Image
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa  (kushoto) na Makamo Mwenyekiti Halmashauri hiyo (kulia) Saidi Ngatipula. .....................................   Halmashauri ya Bagamoyo, mkoani Pwani ,imekusanya zaidi ya sh. bilioni 2.313 sawa na asilimia 85 ya makadirio ya mapato ya mwezi ya sh. bilioni 2.727.6 kwa kipindi cha mwezi septemba mwaka huu.  Makusanyo hayo yanafanya jumla ya makusanyo kutoka mwezi julai hadi septemba kuwa bilioni 6.692.611.969 ambayo ni sawa na asilimia 20 ya makusanyo yaliyokisiwa kukusanywa kwa mwaka.  Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ally Ally Issa wakati akitoa taarifa ya fedha ya mapato na matumizi kwa kipindi cha mwezi septemba, ikiwa ni robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019. Aidha Issa alisema, halmashauri hiyo kwa mwezi septemba imekusanya milioni 159.085.524 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani.  Hata hivyo mwenyekiti huyo ambae pia ni diwani wa kata ya Fu...

NAIBU WAZIRI SUBIRA MGALU ZIARANI MKOANI IRINGA.

Image
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akikata utepe ikiwa ni kuashiria uwashwaji wa umeme katika kijiji cha Igula, Wilaya ya Iringa Vijijini.   Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akibonyesha kitufe cha kuwashita taa na kingora ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa kazi ya kuwasha umeme katika kijiji cha Igula, Wilaya ya Iringa Vijijini. Kijiji cha Igula ni moja ya vijiji vinavyonufaika na mradi wa kupeleka kwenye vijiji vilivyopitiwa na Njia kuu ya Umeme KV 400. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu kabla ya kuzungumza na wananchi na kuwasha umeme katika kijiji cha Igula iliyopo halmashauri ya Iringa Vijijini. Kutoka kushoto ni Katibu tawala, Hashimu Komba na Diwani wa Kata ya Kihologota, Paziyano Kayage. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wanafunzi wa darasa la sita wa Shule ya Msingi Ikengeza iliyopo halmashauri ya Iringa vijijini. Shule hiyo ni miongoni mwa taasisi ambazo zimenufaika na mradi wa kupeleka umeme kwenye v...

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 29, 2018.

Image

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Image

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI WA PALESTINA PAMOJA NA BALOZI WA JAPAN JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Rais)   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Rais)   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Shinichi Goto (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Rais)  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuonyesha viungo vya chai kutoka Zanzibar Balozi wa Japan nchini Mhe. Shinichi Go...

KATIBU MKUU NYAMHANGA AKAGUA DARAJA LA KAVUUU

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende, kuhusu kuifanyia matengenezo barabara ya Majimoto-Inyonga yenye urefu wa KM 130 kwa kiwango cha changarawe, mkoani humo.   Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende, akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), kuhusu ukamilikaji wa Daraja la Kavuu linalounganisha Wilaya ya Mlele na Mpwimbwe mkoani humo. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoka kukagua kingo za Daraja la Kavuu linalounganisha Wilaya ya Mlele na Mpwimbwe mkoani Katavi. Daraja hilo limekamilika na limeanza kutumika kwa magari yasiozidi tani 30. Muonekano wa Daraja la Kavuu le...