MBUNGE wa Jimbo la
Bagamoyo Mkoa wa Pwani Dkt. Shukuru Kawambwa
......................................................
Na Omary Mngindo, Yombo Bagamoyo
MBUNGE wa Jimbo la
Bagamoyo Mkoa wa Pwani Dkt. Shukuru Kawambwa, ameahidi kufuatilia ombi la Wadau
wa elimu, la kutaka kuwepo walimu maalumu wa shule za awali, badala ya kutumika
wa shule za msingi.
Dkt. Kawambwa ametoa kauli
hiyo mwishoni kwa wiki, akizungumza katika kongamano la wadau wa elimu
lililoandaliwa na diwani wa Kata ya Yombo Mohamed Usinga, la kuwapongeza walimu
katani humo, kwa ufaulu mzuri mwaka huu.
Kauli ya Kawambwa
imefuatia ombi kutoka kwa Ofisa Elimu Msingi wilaya ya Bagamoyo Alex Mwakawago,
aliyesema
kuwa walimu wengi
wanaofundisha elimu ya awali ni wa shule za msingi, hivyo walengwa kukosa elimu
inayolingana na umri wao.
"Mheshimiwa Mbunge
tukuombe ulibebe hili, ukakae na wakubwa wenzako kuona ni namna gani serikali
inavyoweka mkakati maalumu, wa kuwepo walimu kwa ajili ya kufundisha madarasa
ya awali, kuliko hivi sasa ambapo wanaofundisha ni wa elimu ya msingi,"
alisema Mwakawago.
Akizungumzia ombi hilo,
Dkt. Kawambwa alisema kuwa ni wazo jema ambalo linapaswa kufanyiwakazi, huku
akiahidi kukutana na Waziri mwenye dhamana ya sekta hiyo, na kuwa anaimani
kubwa kwamba serikali inaweza kulifanyiakazi.
Aidha Dkt. Kawambwa
amewapongeza viongozi ngazi ya Kata wakiongozwa na diwani wao Usinga, kwa
mikakati waliojiwekea katika elimu, kutoka nafasi ya mwisho msimu uliomalizika,
na kushika nafasi za juu mwaka huu.
"Nakumbuka mwaka jana
mlipokea zaeadi ya bendera nyeusi ikiashiria kufanya vibaya katika elimu,
mlikaa mkatafakari wapi mlujikwaa, hatimae mwaka huu mmekuwa wa kwanza kiwilaya
hongereni sana," alisema Dkt. Kawambwa.
Diwani Usinga alisema
kwamva baada yaa kufanya vibaya msimu uliopita walika na kupanga mikaakati
mbalimbali ikiwemo unumuzi wa mashine ya kudurufu karatasi za mithihani, hatua
iliyoboresha ufauli kwenye shule zao.
No comments:
Post a Comment