Diwani wa Kata ya Yombo Wilayani Bagamoyo,
Mohamed Usinga
.......................................................
Na Omary Mngindo, Yombo
SHULE za msingi katika
Kata ya Yombo jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani, kuanzia likizo za mwaka huu
zitafungwa kwa siku moja, zoezi litakalotanguliwa na michezo kwenye
uwanja mmoja.
Diwani wa Kata ya Yombo
Mohamed Usinga aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, akizungumza na walimu katani
humo, mbele ya Mbunge jimbo hilo Dkt. Shukuru Kawambwa, kwenye hafla fupi ya
kuwapongeza kwa kufanya vizuri.
Usinga alisema kuwa hatua
ya kufungwa shule siku moja, kutaendana na ushiriki wa michezo mbalimbali,
hatua itayowezesha wanafunzi na walimu kujumuika pamoja kwenye michezo, kisha
kufungwa siku moja na kufunguliwa pamoja.
"Mheshimiwa Mbunge
ndani ya Kata yetu kwa likizo ya mwaka huu wa 2018 tunataraji kufungwa shule
siku moja, hatua itayotuwezesha kufungwa siku moja, likizo itatanguliwa na
bonanza," alisema Usinga.
Akizungumza hatua hiyo ya
kufungwa kwa kitanguliwa na bonanza, Mbunge Kawambwa alipongeza hatua hiyo,
huku akieleza itaongeza umoja, upendo na mshikamano.
"Niwapongeze walimu
kwa kupandisha ufaulu kwa msimu huu wa masomo, nimepata taarifa kwamba mwaka
jana hamkufanya vizuri hatua iliyosababisha kupewa bendera nyeusi, hongereni
sana," alisema Dkt. Kawambwa.
Kawambwa alisema, kwa
utaratibu wa kushirikisha michezo katika siku za kufunga shule kutawahamasisha
wanafunzi ambao wanapenda michezo, hivyo kuwasogeza katika masomo.
"Nikupongeze Diwani
kwa hatua kubwa mliyopiga katika sekta ya elimu, kwa msimu uliopita katika
elimu mlipata bendera nyeusi kutokana na kutofanya vizuri katika mitihani yenu,
mkajiuliza mwaka huu mmeibuka vizuri kiwilaya na Mkoa," alimalizia Dkt.
Kawambwa.
No comments:
Post a Comment