Posts

Showing posts from July, 2019

MWENGE WA UHURU 2019, WAKAGUA MIRADI 13 HALMASHAURI YA BAGAMOYO

Image
Mwenge wa uhuru 2019, umehitimisha mbio zake katika Halmashauri ya Bagamoyo, kwa kutembelea miradi 13 na kuzindua miradi 2 ambayo ina thamani ya shilingi Bilioni 4.7 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya (KUU), Bi Zainabu Mfaume Kawawa, akiongoza wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, (KUU) wabunge wa   Bagamoyo, Chalinze na viti maalum, wakurugenzi wa halmashauri, watumishi wa serikali, viongozi wa CCM pamoja na wananchi kwa ujumla wakati wa kuaga Mwenge wa Uhuru 2019 mara baada ya kumaliza mbio zake halmashauri ya Bagamoyo.   Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru 2019 kati ya Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa na Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama.

WAZIRI MKUU ATAKA MKANDARASI KUTUMIA VIBARUA WA NDANI YA HALMASHAURI

Image
Na Hadija Hassan, Lindi. Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amemuagiza Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, M/S National Service Construction Department (SUMA JKT ) kutotumia vibarua wanaotoka nje ya Wilaya hiyo na Badala yake wawatumie Vijana waliopo katika Halmashauri hiyo. Majaliwa aliitaka agizo hilo kwa Meja Atupele Mwamfupe Jana baada ya kutembelea na kukagua eneo linalojengwa Ofisi hiyo ambapo alisema kuwa katika eneo hilo wapo Vijana wa kutosha wa watakaoweza Kufanya Kazi kwa uweledi katika ujenzi huo. Hata hivyo Majaliwa alisema ili kuifanya Kazi hiyo iende kwa kasi na kukamilika katika muda uliopangwa Ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za kuwatoa vibarua nje ya Maeneo hayo ni vyema kutumia vibalua waliopo ndani ya Wilaya hiyo. Awali akisoma taarifa ya Mradi huo Mbele ya Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ya Ruangwa, Andrew Chezue alisema kuwa Mrad...

WANACHAMA WA YANGA BAGAMOYO WAFANYA USAFI WA MAZINGIRA.

Image
Na Selestian James. Wanachama wa klabu ya yanga wilayani Bagamoyo wameadhimisha wiki ya wananchi kwa kufanya usafi maeneo mbalimbali ya mji wa Bagamoyo. Shughuli hiyo ya usafi imewajumuisha watu wa kada mbalimbali ambao ni wanachama wa yanga wakiongozwa na Diwani wa kata ya Nianjema   iliyopo katika halmashauri ya wilaya Bagamoyo, Abdul Mzee Pyallah ambaye pia ni katibu wa hamasa ya kuchangia Yanga Bagamoyo. Miongoni mwa sehemu walizofika kufanya usafi ni pamoja na Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo. Shughuli hiyo yenye kauli mbiu "funga kazi kusanya kijiji" ni miongoni mwa hatua muhimu za maadhimisho ya   wiki ya wananchi ambayo ilizinduliwa   visiwani Zanzibar na itafikia kilele mwanzoni mwa mwezi ujao katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Sambamba na hilo Diwani Pyallah pia amezungumzia uwepo wao tena hospitalini hapo siku ya tarehe tatu   ni kwa ajili ya kutembelea wodi ya watoto na kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa. Aidha, ...