Saturday, December 11, 2021

SUBIRA MGALU AKABIDHI MATOFALI NIANJEMA NA MAPINGA

 No description available. 

MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa pwani, Subira Hamisi Mgalu (kulia) akimkabidhi Diwani wa kata ya Nianjema, Abdul Mzee Pyalla matofali kwaajili ya ujenzi wa choo katika shule ya mpya ya sekondari inayojengwa katika kata ya Nianjema Halamshauri ya Bagamoyo.

.........................................................

 

MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa pwani, Subira Hamisi Mgalu, ametoa Tofali 350 kusaidia ujenzi wa vyoo katika shule mpya za kata zinazojengwa Kata ya Nianjema na Mapinga zilizopo Halmashauri ya Bagamoyo  Mkoani humo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi Tofali hizo akiwa kata ya Nianjema Halmashauri ya Bagamoyo, Mgalu alisema anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani kwa kutenga fedha kwa kila Halimashauri ili zitumike kujenga vyumba vya madarasa ambapo kwa kata za Nianjema na Napinga zimetumika kujenga shule mpya za kata ambazo hapo awali hazikuwepo.

Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya fedha hizo zilizotolewa kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo ya sekondari, bado baadhi ya kazi zinahitaaji kutekelezwa na Halmashauri,  wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kufanikisha malengo hayo ambapo yeye Mbunge wa viti maalum, mkoa wa Pwani ambae pia ni mdau wa maendeleo alitoa ahadi ya kuchangia tofali na sasa ametekeleza.

Akielezea baadhi ya kazi ambazo zinahitaji kutekelezwa na Halmashauri,  wananchi na wadau mbalimbali ni pamoja ujenzi wa vyoo,

‘’ Nilipokuja Tarehe 21 mwezi wa 11 nilitoa ahadi ya kuchangia tofali 250 katika shule hii mpya ya Nianjema na Mwenyezimungu amenijaalia leo kutekeleza ahadi yangu’’ Alisema Mgalu.

Alisema mpaka sasa ameshatembelea shule 25 katika Halmashauri za Bagamoyo, Chalinze, Kibaha Mji, Kibaha Vijijini, Kisarawe, na Mkuranga ili kukagua miradi ya maendeleo na kuchangia kwa nafasi yake kama Mbunge anewakilisha Mkoa wa Pwani.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nianjema Abdul Pyalla, amemshukuru Mbunge huyo kwa namna anavyoonyesha ushirikiano wa karibu katika mambo mbalimbali ya maendeleo.

Alisema Mh. Subira Mgalu ni mfano wa kuigwa kwani kwa hatua hii ya ujenzi ilipofikia tayari ameshatembelea mara tatu na hasa ikizingatiwa kuwa ana majukumu ya kutembea mkoa wote wa Pwani na hilo analifanya bila ya kuchoka.

 

Aidha, amewapongeza wananchi wa kata ya Nianjema kwa kujitolea mambo mbalimbali yanayohusu ujenzi huo wa shule mpya ya sekondari katika kata hiyo.

Alisema wananchi wa kata ya Nianjema ni waelewa na wpo tayari kwa kila wanachoshirikishwa kuhusu maendeleo ya kata yao.

Wakati huohuo amewashukuru wadau mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa ni wenye kujitolea hali na mali katika kufanikisha ujenzi huo

Ujenzi huo wa shule Kata za Nianjema na Mapinga unatekelezwa kupitia fedha zilizotolewa na Shirika la fedha la Kimataifa (IMF) kwaajili ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19, ambapo Halmashauri ya Bagamoyo imepokea shilingi Bilioni 1.4

No description available. 

MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa pwani, Subira Hamisi Mgalu akizungumza mara baada ya kukabidhi matofali kwaajili ya ujenzi wa choo  katika shule ya mpya ya sekondari inayojengwa katika kata ya Nianjema Halamshauri ya Bagamoyo.

No description available. 

MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa pwani, Subira Hamisi Mgalu, (kushoto) akipita eneo la ujenzi wa shule ya sekondari Nianjema kukagua kazi inavyoendelea, kulia ni Diwani wa kata ya Nianjema, Abdul Pyalla pamoja na Diwani wa kata ya Kisutu, Awesu Ramadhani.

No description available. No description available. 

MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa pwani, Subira Hamisi Mgalu, (kushoto) akipita eneo la ujenzi wa shule ya sekondari Nianjema kukagua kazi inavyoendelea, nyuma yake ni Diwani wa kata ya Nianjema, Abdul Pyalla pamoja na Diwani wa kata ya Kisutu, Awesu Ramadhani.

No description available.No description available.

MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa pwani, Subira Hamisi Mgalu, akiwa anachapia udongo kwenye moja ya chumba cha darasa katika ujenzi wa shule ya sekondari unaojengwa kata ya Nianjema Halmashauri ya Bagamoyo, Mgalu alifika eneo hilo la ujenzi kukaabidhi matofali yatakayotumika kujenga choo.

Friday, November 26, 2021

WAZIRI AWESO NA DC ZAINAB WAHITIMU SHAHADA ZA UZAMILI.

 No description available. 

Waziri wa maji Mh.Jumaa Aweso na mke wake Mh. Bi Zainabu Abdallah ambaye ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, wakiwa katika picha ya pamoja katika sherehe za kuhitimu shahada zao za uzamili chuo kikuu huria Tanzania, sherehe zilizofanyika jana Kikwajuni Zanzibar.

........................................................

Waziri wa maji Mh.Jumaa Aweso na mke wake Mh. Bi Zainabu Abdallah ambaye ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, wahitimu shahada zao za uzamili (masters) .

 

Wana ndoa hao walikuwa wakisoma masuala ya uongozi na utawala (masters of arts in governance and leadership) toka chuo kikuu huria Tanzania, Mh. Jumaa Aweso ambaye ni mbunge wa Pangani, tayari ana bachelor of science in chemistry toka chuo kikuu cha Dar es salaam. 

 

Kwa upande wa Mh. Bi Zainabu Abdallah yeye tayari alikuwa na Diploma in Customs & Tax Management (DCTM), Bachelor of Business Administration in Accounting (BBA - Accounts)  Postgraduate Diploma in Economic Diplomacy (PGD - ED) Wanandoa hao wamjaaliwa kuwa na watoto watatu.

No description available. 

 Waziri wa maji Mh.Jumaa Aweso na mke wake Mh. Bi Zainabu Abdallah ambaye ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, wakiwa katika picha ya pamoja katika sherehe za kuhitimu shahada zao za uzamili chuo kikuu huria Tanzania, sherehe zilizofanyika jana Kikwajuni Zanzibar.

No description available. 

Waziri wa maji Mh.Jumaa Aweso na mke wake Mh. Bi Zainabu Abdallah ambaye ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, wakiwa katika picha ya pamoja katika sherehe za kuhitimu shahada zao za uzamili chuo kikuu huria Tanzania, sherehe zilizofanyika jana Kikwajuni Zanzibar.

No description available.  

Waziri wa maji Mh.Jumaa Aweso na mke wake Mh. Bi Zainabu Abdallah ambaye ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wao, katika sherehe za kuhitimu shahada zao za uzamili chuo kikuu huria Tanzania, sherehe zilizofanyika jana Kikwajuni Zanzibar.

RAIS DK.MWINYI AFUNGUA MASIKITI WA MASJID AL NOOR UNGUJA UKUU KAEPWANI NA KUJUMUIKA KATIKA IBADA YA SALA YA IJUMAA

 No description available.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Masjid Al-Noor Unguja Ukuu Kaepwani Wilaya ya Kati Unguja na (kulia ) Sheikh Feisal Al Kindi na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Rashid Hadid Rashid, na kujumuika na Wananchi wa Unguja Ukuu katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika msikiti huo leo.

No description available.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Masjid Al-Noor Unguja Ukuu Kaepwani alipowasili katika viwanja vya Msikiti huo kwa ajili ya ufunguzi wake baada ya kukamilika ujenzi wake na kujumuika na Wananchi wa Kijiji hicho katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

No description available.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.,Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kuufungua Msikiti wa Masjid Al-Noor Unguja Ukuu Kaepwani Wilaya ya Kati Unguja na (kulia kwa Rais) Msimamizi wa Ujenzi wa Msikiti huo Sheikh Feisal Al-kindi na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadid Rashid, hafla ya ufunguzi huo iliyofanyika