Zahanati ya kijiji cha Msata iliyopo
kata ya Msata Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo, imeibuka kidedea
kimkoa baada ya kufanya vizuri katika utoaji wa huduma za afya kwa wananchi kwa
kuzingatia matokeo makubwa sasa(BRN) na kufanikiwa kupata nyota nne kati ya
vituo vyote vya afya katika mkoa wa Pwani.
Ushindi huo umepatikana kutokana na
ukaguzi uliofanywa na wizara ya Afya kwa ajili ya malipo kutokana na matokeo ya
huduma kwa matokeo makubwa sasa ,Zahanati ya Msata
ilionekana kukidhi vigezo vilivyowekwa na wizara ya Afya kwa kutoa huduma bora
kwa wananchi kwa kuzingatia matokeo makubwa sasa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Chalinze Bi.Amina
Kiwanuka, aliwapongeza watumishi wa zahanati ya Msata kwa kufanya kazi kwa
kuzingatia vigezo vinavyotolewa na wizara ya Afya na kufanikiwa cheti chenye
nyota tano.
Aidha, Mkurugenzi huyo, amevitaka
vituo vingine vya afya na zahanati katika Halmashauri hiyo kuiga mazuri kutoka
zahanati ya Msata ili kwa ukaguzi ujao vituo vyote vya afya katika halmashauri
ya Chalinze viweze kuibuka kidedea na kupata nyota tano ili kufikia matokeo
makubwa sasa katika sekta ya Afya.
"Mganga Mkuu wa wilaya nakutaka sasa
usimamie utoaji huduma za afya kwa wananchi na uhakikishe vigezo vyote
vinavyotakiwa kwa mujibu wa matokeo makubwa sasa vinazingatiwa na kufanyiwa
kazi." Kiwanuka alisema.
Naye Mganga Mkuu wa halmashauri ya
Chalinze Dkt Rahim Hangai alipokea maelekezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Chalinze na kuahidi kusimamia kwa ukaribu utoaji huduma na
akaongezea na kusisitiza kwa watumishi wote wa afya kuzingatia miongozo ya
wizara ili ukaguzi ujao vituo vyote vya afya vinafikia vigezo na kutunukiwa
cheti cha ufanisi
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa (katikati) akibadilishana mawazo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze, Bi Amina Kiwanuka (kushoto)
kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu.
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akikabidhi vifaa vya Afya katika juhudi
zake za kuwatumikia wananchi walimpigia kra ndani ya jimbo lake.
No comments:
Post a Comment