Thursday, November 8, 2018

MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI AWAOMBA WADAU KUSAIDIA MICHEZO JIMBONI KWAKE.

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Humoud Jumaa akikabidhi zawadi kwa viongozi mbalimbali wa timu zilizoshiriki ligi ya Mansour Cup.
.................................................
Na Omary Mngindo, Ruvu

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Humoud Jumaa amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia michezo jimboni humo.

Jumaa ametoa rai hiyo mwishoni kwa wiki akiwa mgeni rasmi katika fainali ya michuano ya soka ya Mansour Cup, yaliyoandaliwa na Mohamed Mansour, Mjumbe wa Kamati ya Utejelezaji wa (UVCCM) Kata ya Ruvu iliyoshirikisha timu 8.

Alianza kwa kumpongeza Mjumbe huyo kwa kuandaa Ligi hiyo, ambayo imesaidia kuongeza hamasa ya michezo jimboni humo, ambayo imesaidia vijana na wakazi kuwa pamoja na kupata burudani baada ya kazi za ujenzi wa Taifa.

"Nina imani kubwa kwamba katika kipindi chote cha mashindano haya wananchi wote Kata ya Ruvu wamepata burudani safi, pia wamebadilishana mawazo katika kupiga hatua za kimaendeleo, nitumie fursa HII kuwaomva wadau mbalimbali wake jimboni kuandaa madhindano," alisem Jumaa.

Kwa upande wake Mansour alisema kuwa mashindano hayo yalikuwa na ushindani mkubwa, ambayo lengo lake lilikuwa ni kuibua na kiendeleza vipaji vya vijana ndani ya Kata ya Ruvu.

Amezitaja baadhi ya timu zilizoshiriki kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Bingwa na Under 20 Fc ambayo ndio bingwa, Ruvu Sekondari iliyoshika nafasi ya 2, na kwamba ligi hiyo ilishirikisha timu 8.

"Baadhi ya timu zilizoshiriki kwa haraka haraka nazikumbuka 7 ambazo ni 
Kimboza Sc, Kombora Fc, Under 20 Fc,
Ruvu Sekondari, Mnazi United, Veteran Fc ya Ruvu na Academia", alisema Mansour.

Katika kinyang'anyiro hicho timu tatu za juu zipata zawadi mbalimbali ikiwemo kikombe kikubwa, kikombe kidogo, jezi, mbuzi, mipira pamoja, katoni za soda za Azam na miamvuli kwa Kamati za maandalizi wa ligi hiyo
 Mwandaaji wa mashindano hayo bwana Mansour (kushoto) akizungumza jambo na meza kuu.
 
Baadhi ya timu zilizoshiriki michuano hiyo.
 
 
Mashabiki waliofika kushuhudia pambano la mwisho, (Picha zote na Omary Mngindo)

No comments:

Post a Comment