Posts

Showing posts from April, 2024

ULEGA ZIARANI KUKAGUA MIUNDOMBINU ILIYOATHIRIWA NA MAFURIKO MKURANGA

Image
  Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega  leo Aprili 27, 2024 ametembelea maeneo yalioathiriwa na mafuriko ya maji ya mvua katika jimbo la Mkuranga, mkoani Pwani na kufanya tathimini ni kiasi gani maeneo hayo yameathirika na kuona  hatua za kuchukua ili kutatua changamoto hizo. Katika ziara yake hiyo Mhe. Ulega ameanza kukagua maeneo yaliyoathirika na mafuriko hayo ikiwemo barabara na madaraja katika kata ya Mwandege, Tambani, Vikindu, Mkuranga, Kiparang’anda, Mkamba, Kimanzichana, Nyamato na Lukanga. Aidha, ametoa rai kwa wananchi wanaokaa katika maeneo hayo yalioathiriwa na mafuriko kuwa na subira wakati serikali ikiendelea kushughulikia changamoto hizo.

MAGAZETI YA LEO TAREHE 27 APRIL 2024.

Image
 

TRA KAGERA YAVUKA LENGO LA UKUSANYAJI KODI.

Image
  Meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Kagera Castro John Afisa elimu kwa umma TRA Kagera Ruekaza Rwegoshola akitoa elimu ya kodi kwa waandishi wa habari .............................. Na A lodia Babara, Bukoba. Mamlaka ya mapato nchini TRA mkoa wa Kagera imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha Januari hadi Machi 2024 na kufikia asilimia 107. Meneja wa mamlaka hayo mkoa wa Kagera Castro John akizumgumza na waandishi wa habari  Aprili 25, 2024 katika kikao kilicholenga kuhamasisha ulipaji kodi wa hiari pamoja na kueleza mafanikio ya ukusanyaji wa kodi kipindi cha Januari hadi Machi, 2024. "Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Kagera tulipanga kukusanya shilingi bilioni 28.24 lakini tulikusanya shilingi bilioni 30.2 na hivyo kuvuka lengo na kufikia  asilimia 107" amesema John. John ametolea ufafanuzi wa kodi mpya ya bodaboda ambayo inapaswa kulipwa kwa mwaka elfu 65,000 ambapo kila robo mwaka zinapaswa kilipwa shilingi 16,200 na zinalipw...

TaSUBa YAANDAA KONGAMANO LA MUUNGANO.

Image
  Makamo wa Rais wa Serikali ya wanafunzi chuoni hapo, Mwikwabe Msafiri (katikati) akizungumza na washiriki katika kongamano hilo, kulia ni Katibu wa Makamo wa Rais, Cinthia Vincent Lwanda na kushoto ni Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi, Raban Erasto Mbiti. ..................................... Na Athumani Shomari  Bagamoyo. Katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 60 ya Muungano, Serikali ya wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeandaa kongamano la Muungano ambalo limewashirikisha wanafunzi wa chuo hicho na wageni kutoka nje ya chuo. Katika kongamano hilo lililofanyika tarehe 25 April 2024, mada za muungano ziliwasilishwa na kisha kutoa nafasi kwa washiriki kutoa maoni mbalimbali kuhusu Muungano. Washiriki hao walisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao leo unaadhimishwa kwa kutimiza miaka 60 una faida nyingi kwa watanzania wote. Wamezitaja baadhi ya faida hizo ni pamoja ushirikiano wa wananchi wa bara na visiwani katika mambo mbalimbali. W...

MAGAZETI YA LEO TAREHE 26 APRIL 2024.

Image