Sunday, July 30, 2017

IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE MIKOA YA KANDA YA ZIWA

3
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na kikosi cha Polisi wanawake baada ya kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili mkoani Singida, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
 1
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi wa Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Singida, wakati alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
 2
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo na kuwataka wafanyekazi kwa kutenda haki na kusimamia misingi ya sheria na taratibu, IGP Sirro yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
........................
Na Jeshi la Polisi Nchini
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, amemaliza ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na mkoa wa Singida, huku akiacha morali kwa watendaji wa Jeshi hilo hatua ambayo italiwezesha ieshi hilo kufanyakazi zake kwa weledi katika kukabiliana na matishio ya uhalifu na wahalifu.

IGP Sirro, amefanya ziara hiyo ikiwa ni mkakati wake aliojiwekea tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi hilo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa ili kujua namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi.

Katika mazungumzo yake IGP Sirro, amewataka askari na maofisa kutimiza wajibu wao kwa kutenda haki na bila uwoga wala kumuonea mtu muhali jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii.

Hata hivyo, katika mabaraza ya kuzungumza na askari na maofisa baadhi ya hoja kadhaa ziliibuliwa kwa baadhi ya askari waliopata nafasi ya kutoa mawazo yao, ambapo IGP Sirro aliahidi kuzishughulikia mapema ili kuzidisha morari katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Aidha, katika ziara yake IGP Sirro, alipata fursa ya kukutanana Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama ya mkoa huku masuala kadhaa ya kiusalama na mbinu na mikakati ikijadiliwa katika kamati hizo na kuahidi kutoa ushirikiano utakaowezesha kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiuhalifu.

KAWAMBWA NA FAMILIA YAKE WASHIRIKI USAFI WA MAZINGIRA BAGAMOYO.

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa,wa pili kushoto akipanga makundi ya kufanya usafi wa mazingira jana jumamosi Tarehe 29 Julay 2017. katika eneo la Beach Bagamoyo, wa kwanza kulia ni mwanae Maliki Kawambwa na wapili kulia aliyeshika kiuno ni mwanae Mariamu Kawambwa
 
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa,wa pili kushoto na wa kwanza kushoto ni mwanae Mariam Kawambwa wakiwa katika zoezi la usafi wa mazingira maeneo ya Beach mjini Bagamoyo, usafi ulifanyika jana jumamosi Tarehe 29 Julai 2017.
 
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, katikati akizungumza na wananchi eneo la Beach Bagamoyo mara bada ya kumaliza kufanya usafi wa mazingira hapo jana  jumamosi Tarehe 29 Julai 2017, mwenye miwani kulia ni Diwani wa kata ya Magomeni, Mwanaharusi Jarufu, na mwenye miwani kushoto ni Diwani wa viti maalu,Mwambao, Hafsa Kilingo.
.............................

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, ameshiriki usafi wa mazingira na mazoezi ya viungo yeye na familia yake wakiwa wamejumuika na wananchi katika mji wa Bagamoyo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya viungo pamoja na usafi wa mazingira, Kawambwa alisema ameamua kuifanya kuwa siku rasmi kujumuika na wananchi wake katika kumuunga mkono Rais john Magufuli kuhusu swala la usafi wa mazingira.

Alisema jamii inapaswa kujenga tabia ya kufanya usafi wa mazingira ili kuepuka magonjwa yenye kuambukiza kama kipindupindu.

Alisema kufuatia umuhimu huo ndiomana hata yeye ameweza kutoka na watoto wake Mariam na Maliki ili nao washiriki usafi wa mazingira katika jamii na kwamba waone umuhimu wa kushirikiana na watu wa aina zote katika mambo mbalimbali ya kijamii.

Katika zoezi hilo la usafi alipata fursa ya kuzungumza na wavuvi na wauza samaki katika ufukwe wa Bahari ya hindi Bandari ndogo ya Bagamoyo.

Awali wavuvi walimueleza mbunge Kawamba kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa soko la kuuzia samaki hali inayopelekea kukaa juani na kunyeshewa 

Kawambwa aliwaeleza wavuvi hao kuwa hivi karibuni soko la kuuzia samaki litakamilika ili kuwaondolea adha ya kuhangaika na sehemu ya kuuzia samaki.

Katika Bonanza hilo la usafi vikundi vya Jogging kutoka Dar es Salaam vikiongozwa na Uhuru Jogging kutoka Radio Uhuru viliungana vikundi vya Jogiging vya Bagamoyo ili kutekeleza usafi kwa Pamoja ikiwa ni ishara ya kujenga ujirani mwema kati ya vijana wa Dar es Salaam na Bagamoyo, ambapo kwa Bagamoyo wenyeji wao walikuwa ni Bagamoyo Jogging.
 
 vijana wa Joging wakiwa katika zoezi la usafi mjini Bagamoyo
 
 Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, katikati akiwa ameungana na wananchi wake katika kufanya mazoezi ya kukimbia kala usafi hapo jana jumamosi Tarehe 29 Julai 2017
 
   vijana wa maigizo wakimunyesha Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa, igizo linaloonyesha madhara yatokanayo na uchafu.