Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chupa yenye ujazo wa nusu lita yA mkojo wa
sungura wakati alipotembelea banda la wanawake wajasiriamali wasindikaji wa
Tabora katika maonyesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji katika Mkoa
wa Tabora yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora,
Novemba 21, 2018. Kwa mujibu wa Mratibu wa Wajasiriamali hao, Bibi Ashura
Mwazembe, mkojo wa Sungura unatumiwa kama mbolea ya mazao ya kilimo na pia ni
dawa nzuri sana
ya kuua wadudu waharibifu wa mazao. Lita moja ya mkojo huo inauzwa sh. 10,
000/=. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Jukwaa la Fursa za
Biashara na Uwekezaji mkoani Tabora kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo,
Novemba 21, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Imani Matabula
(kulia) kuhusu sabuni zinazotengenezwa na Kampuni yake ya Matabula Soap
Investment ya Kaliua mkoani Tabora katika maonyesho ya Jukwaa la
Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora yaliyofanyika kwenye viwanja vya
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa
huo, Aggrey Mwanri.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sabuni za Kampuni ya Matabula Soap Investment
ya Kaliua mkoani Tabora, Imani Matabula (kulia) katika
maonyesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21,
2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanri. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa
wa Tabora, Aggrey Mwanri na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Imani
Matabula.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Saidi Kanimba
kuhusu viatu vya ngozi vinavyotengenezwa katika Halmashuri ya wilaya
Uyui mkoani Tabora katika Maonyesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na
Uwekezaji Mkoani Tabora yailyofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Tabora, Novemba 21, 2018. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey
Mwanri.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakisalimina na Kaimu Mhariri Mtendaji
wa Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah (kushoto) wakati
alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Tabora kushiriki katika
Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora, Novemba 21, 2018.
Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.
No comments:
Post a Comment