Posts

Showing posts from February, 2024

MILIONI 800 KUWASAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO MULEBA.

Image
  Na Alodia Babara  Bukoba, Walengwa wapatao 482 walioathirika na mafuriko pamoja na upepo mkali  katika wilaya za Muleba na Manispaa ya Bukoba mwaka jana wanatarajia kupata msaada wa kibinadamu wenye malengo mbalimbali utakaoghalimu zaidi ya sh. milioni 800 kutoka taasisi zisizo za kiserikali. Msaada  huo ambao unatolewa na Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi kwa ufadhili wa taasisis inayojihusisha na shughuli za kibinadamu kwa watu wenye majanga nchini Tanzania (TCRS) na taasisi ya Actalliance Tanzania Forum utakuwa wa mwaka mmoja utawezesha kutimiza malengo sita ambayo ni msaada wa chakula, uboreshaji wa makazi, msaada wa kisaikrojia, huduma za maji, elimu na Afya na usafi wa mazingira. Akizindua mradi huo Februari 19, mwaka huu mkuu wa mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa alisisitiza mambo matatu ikiwemo  matumizi ya fedha za walengwa, usimamizi mzuri pamoja na  elimu ya maafa kwa walengwa. ...

DIVISHENI YA ELIMU SEKONDARI YAFANYA KIKAO KAZI CHALINZE.

Image
  Divisheni ya Elimu Sekondari katika Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, imefanya kikao kazi kufanya tathmini ya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya matokeo ya kidato cha pili na cha nne kwa mwaka 2023 ili kuweka mikakati mbalimbali katika kuboresha utendaji kazi ili kufikia Malengo ya utendaji kazi (Key Performance Indicators). Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 19 Februali 2024 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo katika Halmashauri hiyo na kuhusisha Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali na binafsi na walimu wa Taaluma katika Shule zote za Sekondari katika Halmashauri ya Chalinze. Akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi Afisa Elimu wilaya ya Chalinze, Bi Salama Ndyetabura alieleza mafanikio na Changamoto mbalimbali zinazoikabili Divisheni ya Elimu Sekondari, huku akiishukuru Halmashauri ya Chalinze kwa kuweza kujenga maabara kwa baadhi ya Shule za Sekondari katika Halmashauri hiyo Afisa Elimu Sekondari, ametoa pongezi kwa wakuu wa...

MIZIGO YAONGEZEKA BANDARI YA MTWARA

Image
 N a Albert Kawogo, Mtwara BANDARI ya Mtwara imeongeza kiasi cha mizigo inayohudumiwa hapo kutoka kiasi cha tani laki nne hadi tani milioni 1.6 katika kipindi cha mwaka 2022/2023. Chachu ya ongezeko hilo linatokana na hatua kubwa ya kimkakati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA kufanya maboresho yenya thamani ya shilingi bilioni 157.8 kwenye eneo la gati ya bandari hiyo sambamba na ununuzi wa mtambo wa kupakia na kushusha mizigo. Ferdinand Nyathi meneja wa Bandari ya Mtwara amewaeleza wahariri wa habari  kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) waliotembelea bandari hiyo kuwa,  jitihada kubwa zinazofanywa na TPA kwenye uwekezaji wa miundombinu ya bandari ndio zinaongeza ufanisi katika utendaji. "Uwekezaji  umeimarishaji  mifumo ya bandari na matunda ya kazi hii ni kwamba msimu wa korosho ambao sasa uko mwishoni tumeweza kuhudumia meli kubwa 28" Alisema Nyathi Nyathi aliendelea kufafanua kuwa Bandari hiyo imekuwa ikisafirisha makaa ya mawe, saruji ya ...

RAIS SAMIA ASIKITISHWA NA MAUAJI YA PALESTINA.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inasikitishwa na vita vinavyoendelea Palestina vinavyosababisha mauaji ya watoto na raia wasio na hatia. Rais Samia ameyasema hayo Tarehe 07 february 2024 katika sherehe za mwaka mpya 2024 (Diplomatic Sherry Party) kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya kimataifa zilizofanyika Ikulu jijini Dar es salaam. Aidha, amesema Tanzania inaunga mkono usuluhishi kati ya Palestina na Israeli kwa kutoa wito wa kusitisha mapigano na kupatiwa misaada ya kibinadamu. Wakati huohuo Rais Samia amesema Haki, Demokrasia, Sheria na Utawala bora vitadumishwa kwa watu wote wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Amesema ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, kikosi kazi huru cha kupitia na kushauri mageuzi muhimu katika mfumo wa siasa kiliundwa ambapo kiliwasilisha ripoti yake mwaka 2023 Rais Samia pia amesema mapendekezo mengi ya...

UWT NA KIPAUMBELE CHA MAZINGIRA WEZESHI KUINUA WANAWAKE KIUCHUMI

Image
  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Doto Biteko akimkabidhi Nakala ya Makubaliano kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda (MCC) jijini Dodoma Tarehe 07 February 2024. ....................... DODOMA  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Doto Biteko  amemkabidhi Nakala ya Makubaliano kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)  kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda (MCC) katika Hafla ya Utiaji Saini wa Makubaliano hayo. Aidha, Mwenyekiti Chatanda alishiriki hafla hii kwa lengo la kuhakikisha UWT inakuwa mstari wa mbele katika kuchangia uwepo wa mazingira wezeshi ya kuwainua Wanawake Kiuchumi kuanzia katika utoaji elimu na hamasa kwa jamii. UWT IMARA JESHI LA MAMA SAMIA KAZI IENDELEE.

ALIYEMKATA KIGANJA KATIBU WA BAKWATA BUKOBA AUWAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA.

Image
  Na Alodia  Babara Bukoba, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la A bdulmalick Yahya (42) mkazi wa wilaya ya Muleba ambaye alikuwa mtunza ghala katika mradi wa ujenzi wa BAKWATA Bukoba (BAKWATA COMPLEX) amefariki baada ya kushambiliwa na wananchi wenye hasira kufuatia tukio alilofanya la kumshambulia katibu wa BAKWATA wilaya ya Bukoba na kumkata kiganja cha mkono. Katibu wa Bakwata wilaya ya Bukoba Hamza Zakaria (43) akiwa anaendelea na matibabu katika hospital ya rufaa ya mkoa, Bukoba amesimulia alivyoshambuliwa na aliyekuwa mtunza ghala la ujenzi wa BAKWATA Complex na kuanza kumkata kwa panga kisha kutenganisha kiganja na kiwiko cha mkono wa kushoto. "Ilikuwa ni majira ya saa 10:00 asuhuhi siku ya Tarehe 2 februali 2024 wakati nikiwa kazini kwangu nilitoka kwenda duka la jirani kuangalia viatu kwa mtu mmoja anaitwa Khalid ndipo alitokea Abdulmalick Yahya akiwa ameshika panga na kuanza kunishambulia" amesema Hamza Ameendelea kusimulia kuwa, alipomkata panga la kwanza ali...

HATUTAWAFUMBIA MACHO WANAOJIITA BOKO HARAMU NDANI YA MKOA WA PWANI - Mramba

Image
  Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Pwani ndg David Mramba amesema hawako tayari kuwafumbia macho wanaojiita boko haramu kwani kujiita hivyo ni kuhatarisha maisha ya Watanzania. Mramba ameyasema hayo leo tarehe 06/02/2024 katika Ofisi za CCM Mkoa wa Pwani kuwa CCM ina macho mengi hata mtu akiwa kwenye shimo ataonekana na akibainika hataachwa salama kimaadili. Amesema wako watu wanataka kuwatishia Wanaccm kwa kujiita wao ni boko haramu jambo ambalo si jema ndani ya CCM. " Unapojiita boko haramu tafsiri yake wewe ni mtekaji na mbakaji hivyo lazima tuwashughulikie watu wa aina hiyo  amesema Mramba Ameendelea kusema kuwa hakuna kikundi ndani ya CCM kitakachokuwa na uwezo wa kubadili mawazo ya Wanaccm kwa kuwatishia. Amesema wako wanaowatishia Viongozi walioko madarakani wakidai kuanza kutengeneza safu zao huku wakijipachika majina ya aina hiyo. Hatutawavumilia wanaokiuka taratibu za Chama na tuko tayari kuwaadhibu ili Chama na wanachama wabaki salama  amesema ...

WAFANYABIASHARA WA MAFUTA ZINGATIENI MAISHA YA WANANCHI - DKT. BITEKO

Image
  Na Mwandishi wetu, Dodoma Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama cha Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta nchini (TAOMAC) ambapo amewataka wafanyabiashara hao pamoja na faida wanayoipata wazingatie maslahi wananchi wa hali ya chini. Ameyasema hayo tarehe 06 Februari, 2024 jijini Dodoma katika kikao ambacho kilijadili masuala mbalimbali ikiwemo changamoto mbalimbali ambazo wanafanyabiashara hao wanazikabili. Amesema Serikali siku zote iko tayari kutoa ushirikiano kwa wafanyabiashara na kuwekea mazingira wezeshi ya biashara zao ili waweze kuwajibika kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu za usimamizi katika sekta husika. “Tunapofanya biashara hii ya mafuta lazima tuangalie mtanzania maskini ambaye anategemea sekta hii kujikwamua kimaisha, isifike mahala kila mwisho wa mwezi watu wote wanashika vichwa wakihofia kupanda kwa bei ya mafuta… Serikali inafanya kila jitihada kupunguza makali ya bei ya mafuta hi...

TAKUKURU KAGERA YABAINI MAPUNGUFU KATIKA MIRADI 16.

Image
  Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera Pilly Mwakasege akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu  Octoba hadi Desemba 2023 .................................. N a Alodia Babara Bukoba TAASISI ya kuzuia na kupamba na Rushwa mkoa wa Kagera kwa kipindi cha Oktoba-Desemba 2023, imefuatilia miradi 19 yenye thamani  zaidi ya shilingi bilioni 6.1 ambapo kati ya hiyo miradi 16 yenye thamani zaidi ya shilingi bil.4.2 imebainika kuwa na mapungufu yaliyohitaji marekebisho. Kamanda wa taasisi hiyo mkoani humo Pilly Mwakasege amesema kuwa kiasi hicho ni sawa na asilimia 68.50 ya fedha za miradi ambapo kumekuwa na ongezeko la asilimia 18.77 ya miradi hiyo, ukilinganisha na kipindi cha Julai-Septemba mwaka jana. Mwakasege ameeleza hayo leo Februari 06,2024 wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi cha robo tatu ya mwisho wa mwaka 2023 ambapo,miradi iliyohusika ni ya ujenzi wa miundombinu ya shule mpya za msingi na sekonda...

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA MSD

Image
  Na. WAF, Dodoma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI imeitaka Bohari ya Dawa (MSD) kuongeza ufanisi, ubunifu wa hali ya juu kwa kuhakikisha dawa zinanunuliwa, zinahifadhiwa sehemu sahihi, kusambaza dawa hizo kwa wakati katika sehemu zenye uhitaji na kukusanya madeni ili kuweza kuwa imara na taasisi endelevu. Wito huo umetolewa leo Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI, Mhe. Stansilaus Nyongo baada ya kupokea taarifa ya hali ya utendaji na majukumu ya Bohari ya Dawa (MSD). Mhe. Nyongo amesema kuwa wao kama wawakilishi wa wananchi wataendelea kuishinikiza serikali kuiwezesha MSD kupata mtaji ili kujiendesha kiufanisi katika kusambaza dawa kwa wakati. “Bohari kuu ina majukumu ya kununua, kutengeneza, kuhifadhi dawa pamoja na kusambaza dawa katika vituo vya  vyote nchini”. Ameeleza  Mhe. Nyongo. Mhe. Nyongo amesema kwa ujumla kamati imeridhishwa na hali ya utendaji wa Bohari ya Dawa na mipango yake ya utek

PWANI YAHITIMISHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 47 YA KUZALIWA KWA CCM

Image
  Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani leo tarehe 04/02/2024 kimehitimisha sherehe za  Maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM katika Kata ya  FUKAYOSI Wilaya ya  Bagamoyo huku kikiwa na matumaini makubwa ya ushindi kuelekea uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa, Vijijini na Vitongoji 2024. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika kuhitimisha maadhimisho hayo ndg. Mwinshehe Mlao amesema ili CCM iweze kuendelea kudumu lazima Viongozi waondoe ubinafsi. Mlao amesema unapofika wakati wa uchaguzi Kila mpiga kura ahakikishe anawachagua Viongozi wa Serikali wenye nia njema ya kuongoza na ikitokea  wakawachagua Viongozi kwa ajili ya maslahi yao binafsi basi watakuwa wamepoteza haki za wengine. Ameendelea kusema kuwa ili kushinda chaguzi zijazo kunahitajika UMOJA huku akisisitiza kuwa kama Kuna mwanachama yeyote mwenye nia ya kugombea na anaonekana kuwa na dosari aambiwe sasa wasisubiri mpaka achukue fomu ndio waseme mabaya yake huko ni ...

LIONS CLUB YAKABIDHI MATENKI YA MAJI CHALINZE.

Image
  MUNTAZIR Bharwan mmoja wa Wanachama wa Taasisi ya Lions Club, akielekeza jambo mbele ya Diwani wa Kata hiyo Mussa Gama mwenye Balaghashia. Picha na Omary Mngindo. Miriam Kihiyo (Watatu kutoka kwa aliyevaa Balaghashia) akimkanidhi moja ya zawadi mtoto anayetoka kwenye Kituo cha kulelea Watoto wenye Mazingira hatarishi. Picha na Omary Mngindo. .................................... Na Omary Mngindo, Ruvu. TAASISI ya Lions Club ya jijini Dar es Salaam imekabidhi matenki 8 ya kuhifadhia maji katika shule za msingi na Sekondari ndani ya Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani. Matanki hayo yanalenga kuwaondolea adha wanafunzi kwenye shule hizo, yamekabidhiwa kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Chalinze, Ramadhani Possi, aliyewakilishwa na Miriam Kihiyo Afisa Elimu Msingi. Muntazir Bharwan alisoma taarifa ya taasisi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Lions Host Kaniz Naghavi, iliyoeleza kuwa kukabidhiwa kwa matenki hayo kumetokana na diwani wa Kata hiyo Mussa Gama kuelezea uwe...

DED BAGAMOYO AZINDUA HUDUMA KITUO CHA AFYA FUKAYOSI.

Image
  Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bw. Shauri Selenda Leo tarehe 1 Februari, 2024 amezindua rasmi utoaji wa huduma katika kituo Cha Afya Fukayosi. Akizungumza na watumishi wa Afya pamoja na Kamati ya Maendeleo ya Kata Fukayosi (WARDC) Selenda, alisisitiza kufanya kazi Kwa weledi pamoja na  kunyenyekea wagonjwa kama sehemu ya miiko ya tasnia ya utoaji wa huduma za afya. " Mgonjwa mpaka anafika hospitali maana yake anahitaji huduma hivyo haina budi kumpokea kwa unyenyekevu na kumsikiliza shida yake na kumpatia matibabu". Alisema Bwana Selenda.            Kituo Cha Afya Fukayosi kimejengwa kwa kutumia fedha toka Serikali Kuu na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa lengo la kuimarisha huduma za afya ikiwemo Huduma ya Mama na Mtoto, Afya ya dharura na upasuaji wa wajawazito, Maabara, Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD), Mionzi, na Jengo la kufulia. Mkurugenzi Mtendaji alipanda miti kama i...

DC. OKASH ATATUA KERO ZA BODABODA BAGAMOYO.

Image
  Na Daria Abdul, Hamisi Hamisi, Bagamoyo. Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okash, akishirikiana na  viongozi mbalimbali wa Halmashauri  ya Wilaya hiyo, amefanya kikao na madereva wa pikipiki zinazobeba abiria (BODABODA)  Januari 31,2024 katika ukumbi wa flexible hall Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA), kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili katika utendaji kazi wao wa kila siku.  Mhe.Okash, amewasisitiza bodaboda kutii sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali, pia wajiepushe na matukio ya uhalifu wa kupora mali za wateja wao. ”Ndugu zangu lazima tutii sheria za usalama barabarani kwani tunawategemea ninyi vijana kuwa ndio Taifa la kesho hizo rizki tunazozipata kuna watu wanatutegemea tusipotii sheria za usalama barabarani, kutakuwa na ajali za mara kwa mara zitakazopelekea kupoteza maisha na kuleta ulemavu.” Amesema Okash Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Usalama barabarani,  Wilaya ya Bagamoyo (DTO)  Azizi...

WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUTUMIA FEDHA ZA TASAF KUJIENDELEZA KIMAISHA.

Image
  Mkurugenzi wa uratibu  wa shughuli za serikali ofisi ya makamu wa pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Siajabu Suleiman Pandu akizumgumza na wanufaika wa mpango wa TASAF Manispaa ya Bukoba hawako pichani. .......................................... Alodia Babara, Bukoba. WALENGWA wa mpango wa kunusuru kaya maskini nchini, TASAF wametakiwa kuzitumia fedha za mpango huo kama sehemu ya ukombozi, kuimarisha ndoa na familia zao kwa lengo la kuondoa umaskini. Hayo yamesema Januari 31, mwaka huu 2024, na Mkurugenzi wa uratibu wa shughuli za serikali ofisi ya makamu wa pili wa Rais Zanzibar Siajabu Pandu wakati wadau mbalimbali wa mpango huo walipotembelea walengwa katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kwa lengo la kukusanya maoni na changamoto zinazowakabili walengwa, ambazo baada ya kuzibaini zitawawezesha wadau hao kuboresha mpango unaofuata. “Serikali tunaamini fedha hii iwe ni sehemu ya ukombozi, kwa hiyo ninawaomba muishi katika ndoa njema, familia nzuri ni se...