Meneja
wa TCRA Kanda ya Kaskazini Fransis Msungu akiongea kwenye semina
iliyowashirikisha watendaji wa kata na mitaa waalimu wakuu kutoka halmashauri
za jiji na wilaya ya Arusha sanajri na wakuu wa vituo vya polisi wilayani hapa
iliyofanyika kwenye hotel ya Golden Rose jijini hapa picha zote na mahmoud
ahmad arusha.
......................................
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)imewataka
wale wote wenye kuuza bidhaa za mawasiliano ikiwemo simu za mkononi,Radio na
Runinga kuhakikisha wanajisajili kwao ili wananchi wapate huduma zilizo sahihi
na kuondoa malalamiko kutopata huduma stahiki.
Akizungumza kwenye semina ya huduma za utangazaji
kwa channeli zinazotazamwa bila malipo iliyowashirikisha watendaji wa
mitaa,Kata, Wakuu wa vituo vya polisi,waalimu wakuu wa shule sanjari na
watumisha wa idara za serikali wilayani hapa Meneja wa mamlaka hiyo
Mhandisi
Fransis Msungu amesema kuwa hapa Arusha mamlaka hiyo imebaini kuwa
wafanyabiashara wengi wana leseni za biashara lakini za mamlaka hiyo wengi wao
hawana.
Amesema kuwa maswali mengi yalioelekezwa kwa
mamlaka hiyo imeonyesha mafundi wa simu na maduka mengi hayana leseni za
mamlaka hiyo hivyo kutoa wito kwao kuangalia na kujisajili haraka kwao ili
kuweza kumlinda mlaji.
“Nawasihi wote kuhakikisha wanajisajili haraka
kwao ili kuwezakuondoa malalamiko yanayotolewa na walaji kwa mamlaka yetu
utaona hapa Arusha kuna maduka 40 yenye leseni zetu mengi yaliopo bado
hayajasajiliwa sanjari na mafundi wa simu”alitanabaisha Msungu.
Kwa Upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha
David Mwakiposa amesema kuwa mbali na malalamiko mbali mbali yaliotolewa na
washiriki wa mkutano huo suala zima ni mashirikiano kati ya Tcra na wadau
mbalimbali na semina hiyo imefungua milango kwa wananchi kwani elimu itawafikia
walengwa ambao ni wananchi.
Amesema kuwa semina hiyo inatakiwa kuwa endelevu
na watendaji wamejipanga kuhakikisha kuwafikishia wananchi kwenye maeneo yao na
tutarajie kuondoa changamoto mbali mbali zinazo wakabili wananchi hususani ya
wizi wa mtandao.
“Natoa rai kwa TCRA kuhakikisha changamoto mbali
mbali zinazoelekezwa kwao kuzitafutia ufumbuzi ili kuondoa kero na adha
wanayokutana nayo wananchi katika maeneo mbali mbali hapa nchini tunashukuru
sana sisi tumepata uelewa wa masuala haya ya channel zisizolipiwa na tunaahidi
kutoa elimu kwa wananchi”alisema Mwakiposa
Aidha Baadhi ya washiriki mbali mbali walioshiriki
katika semina hiyo wamepata uelewa ila wakaitaka Tcra kuenda mbele zaidi katika
suala zima la utoaji wa elimu kwa wananchi sanjari na kutatua changamoto mbali
mbali wanazokutana nazo walaji wa mamalaka hiyo.
Muwasilishaji
kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini Tcra Janny Kaaya akitoa mada wakati wa
semina ya watendaji wa kata na mitaa waalimu wakuu na wakuu wa vituo vya polisi
walioshiriki semina hiyo kwenye hotel ya Golden Rose jijini hapa picha na
mahamoud ahmad wa globu ya jamii arusha
Katibu
tawala wa wilaya ya Arusha mjini David Mwakiposa akifunga semina hiyo
iliyowashirikisha Halmashauri za jiji la Arusha na wilaya ya Arusha
iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Rose jijini hapa picha na mahmoud ahmad wa
globu ya jamii Arusha.
No comments:
Post a Comment