Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa (kushoto) na Makamo Mwenyekiti Halmashauri hiyo (kulia) Saidi Ngatipula.
.....................................
Halmashauri ya Bagamoyo,
mkoani Pwani ,imekusanya zaidi ya sh. bilioni 2.313 sawa na asilimia 85 ya
makadirio ya mapato ya mwezi ya sh. bilioni 2.727.6 kwa kipindi cha mwezi
septemba mwaka huu.
Makusanyo hayo yanafanya
jumla ya makusanyo kutoka mwezi julai hadi septemba kuwa bilioni 6.692.611.969
ambayo ni sawa na asilimia 20 ya makusanyo yaliyokisiwa kukusanywa kwa
mwaka.
Hayo yalibainishwa na
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ally Ally Issa wakati akitoa taarifa ya fedha
ya mapato na matumizi kwa kipindi cha mwezi septemba, ikiwa ni robo ya kwanza
ya mwaka wa fedha 2018/2019.
Aidha Issa alisema,
halmashauri hiyo kwa mwezi septemba imekusanya milioni 159.085.524 kutoka
vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani.
Hata hivyo mwenyekiti huyo
ambae pia ni diwani wa kata ya Fukayosi alisema, mapato ya septemba
yameongezeka ukilinganisha na mapato ya mwezi agost mwaka 2018.
Issa alisema, kipindi cha
mwaka wa fedha 2017/2018 ilikisia kutumia bilioni 32.371.697.034 .
“Kiasi cha 368.958.970
zilivuka mwaka wa fedha 2017/2018 ,kiasi hicho kitakuwa ni sehemu ya matumizi
kwa kipindi cha 2018/2019 hivyo kufanya jumla ya matumizi kwa mwaka wa fedha
2017/2018 kuwa bilioni 33.100.926.004”
Akizungumzia mikakati
waliyonayo katika kipindi cha 2018/2019 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa alisema ni
kuhakikisha kwamba wanasimamia mapato na matumizi ili kulenda maendeleo katika
Halmashauri hiyo.
Alisema kwa sasa
Halmashauri hiyo imejipanga kuboresha vyanzo vya mapato ili kuongeza kasi ya
ukusanyaji.
Aidha, aliongeza kuwa,
tayari Halmashauri imeshapata eneo litakalojengwa kituo kikubwa cha mabasi
yaendayo mikoani na kwamba kituo itakuwa ni sehemu ya kukusanyia mapato.
Madiwani wa Halmashauri ya
Bagamoyo wakiwa katika kikao cha Baraza
Madiwani wa Halmashauri ya Bagamoyo wakiwa katika kikao cha Baraza
No comments:
Post a Comment