Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Angellina Mabula akijibu swali wakati wa kikao cha pili
cha Mkutano wa 13 wa Bunge jana Novemba 07, 2018 jijini Dodoma.
..................................................
Serikali imeendelea kuchukua hatua za
kubatilisha milki za ardhi za mashamba yaliyotekelezwa katika maeneo mbalimbali
nchini.
Hayo yamesema Bungeni leo na
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula
wakati akijibu swali la Mhe. Dustan Kitandula Mbunge wa Mkinga kuhusu kufuta
hati za mashamba yaliyotelekezwa.
“Katika kipindi cha Disemba, 2015
mpaka Octoba, 2018 mashamba yenye ukubwa wa ekari 84,240.803 yamebatilishwa
katika Halmashauri za Ngorongoro, Arumeru, Moshi, Kinondoni,(Manispaa),
Kigamboni(Manispaa), Mvomero, Kilombero, Kilosa, Mvomero, Iringa, Bukoba,
Tarime, Kibaha, Serengeti, Busega, Muheza, Lushoto na Mkinga” amefafanua Naibu
Waziri Mabula.
Mabula anasema kuwa, katika
Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Shamba Na. 278 Mkomazi lenye ukubwa wa ekari
15,442 lililokuwa likimilikiwa na kampuni ya M/S Mkomazi Plantations Limited
kwa Hati Namba 4268, 9780 na 9781 milki yake ilithibitishwa tarehe 20
Juni, 2018.
Aidha anafafanua kuwa, baada ya
kubatilishwa kwa milki ya shamba hilo, Serikali ya Mkoa wa Tanga kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga zipange matumizi mapya ya
shamba hilo kwa kuzingatia mahitaji ya ardhi katika eneo hilo kipaumbele kikiwa
ni mahitaji ya wananchi na ardhi kwa ajili ya uwekezaji.
Mbali na hayo Mabula amezitaka
Halmashauri zote nchini kubaini mashamba yaliyotelekezwa kutuma ilani kwa
wamiliki wa mashamba hayo kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi (Sura 113) na
kuwasilisha mapendekezo katika Wizara ya Ardhi kwa hatua za kubatilisha milki
za mashamba hayo ziweze kufanyika.
No comments:
Post a Comment