Posts

Showing posts from February, 2019

WANAOINGIZA MABINTI WA SHULE GESTI SASA KUKIONA...TGNP YAOMBA MSAADA KWA...

Image

Waziri Kamwelwe asifu utendaji kazi wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania

Image
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi. Isack Kamwele amepongeza utendaji kazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Mhe. Kamwele alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea Ofisi za TMA, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, tarehe 27 Februari 2019 na alipata taarifa ya utendaji kazi wa mamlaka na kutembelea baadhi ya sehemu za kazi kabla ya kuzungumza na wafanyakazi. Mhe. Kamwele alipokelewa na uongozi na menejiment ya TMA, ikiongonzwa na mwenyekiti wa bodi ya ushauri Dkt. Buruhani Nyenzi na kaimu mkurugenzi mkuu Dkt. Ladislaus Chang’a. Kat “Nawapongeza TMA kwa umakini na utekelezaji wa majukumu yenu, nakiri kusema ni moja ya taasisi makini kati ya taasisi zilizo chini ya wizara yangu nilizo tembelea”. Alizungumza mhe. Kamwele Aidha, mhe. Kamwele alisisitiza kuboresha mfumo wa ushirikishwaji wa wadau na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa, akitolea mfano mafuriko yaliyo bomoa barabara eneo la Dumila, kuwa baada ya kufuatilia taarifa za hali ya hewa waligu...

DC BAGAMOYO ATAKA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA WOTE KURIPOTI SHULE IFIKAPO JUMATATU MACH 04.

Image
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa,  akishiriki ujenzi wa vymba vya madarasa shule ya sekondari Pera Halmashauri ya Chalinze, aliyesimama kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Saidi Zikatimu. ............................ Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka shule watoto wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza ifikapo jumatatu ya tarehe 04 Mach 2019. Mkuu huyo wa wilaya ametoa tamko hilo wakati akizungumza na viongozi wa kata na tarafa katika Halmashauri ya Chalinze na kuwataka viongozi hao wasimamie maagizo hayo. Tamko hilo limekuja baada ya shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa zikiendelea wilaya yote ya Bagamoyo lengo likiwa ni kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakaekosa masomo kwasababu ya upungufu wa vyumba vya madarasa. Katika ziara yake hiyo ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, Mkuu huyo wa wilaya ameshiriki shughuli za ujenzi katika shule ya Sekondari Pera kata y...

NAPE APONGEZA KUWASHWA UMEME KIJIJI CHA TULIENI, LINDI.

Image
NA HADIJA HASSAN, LINDI. Kuzinduliwa kwa Umeme , kupitia mradi wa Umeme Vijijini (REA) katika Kijiji cha Tulieni kata ya Mtua Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani humo kunaweza kuwa Mwarobaini wa kumaliza changamoto ya upatikanaji wa Maji  inayowakabili wananchi kijijini hapo Hayo yameelezwa na Mbunge Jimbo la Mtama Nape Nnauye wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa uwashaji wa umeme katika kata hiyo uliofanyika jana katika ofisi za  kijiji cha  Tulieni   na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji hicho Nape alisema kuwa kutokana na Kijiji  kuwa mlimani wakazi wa maeneo hayo hulazimika kushuka chini (mabondeni) kufuata huduma ya Maji katika mifereji na mito ambayo hata hivyo sio salama kwa afya zao " Wakati wa Kampeni za uchaguzi mwaka 2015 kijiji hiki kilikuwa na Matatizo Makubwa mawili , moja bara bara ambalo limeshaanza kufanyiwa kazi na wakala wa bara bara mijini na vijijini (TARURA ) kwa kujenga...

MAGAZETI YA LEO 28 FEB. 2019.

Image

Uzinduzi wa kampeni ya ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili wa kingono wafana dar…viongozi wa dini, jamii yaombwa kumlinda mtoto

Image
  Maandamano... sehemu ya washiriki katika Kampeni ya ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili wa kingono- “1-5-5 namlinda” yenye kauli mbiu “ mlinde mtoto afurahie utoto wake, ujana wake na uzee wake” wakionyesha mabango yao Mgeni katika shughuli hiyo, Mkuu wa Dawati la kijinsia kutoka makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, DCP  Maria  Nzuki akielezea jambo katika Kampeni hiyo. Mkurugenzi mtendaji Lilian Liundii akifafanua jambo Mkurugenzi akiiwa na mgeni rasmi katika kampenii hiyo.   Na Selemani Magali Kampeni ya ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili wa kingono- “1-5-5 namlinda” yenye kauli mbiu “ mlinde mtoto afurahie utoto wake, ujana wake na uzee wake” imezinduliwa jana huku viongozi wa kidini na jamii kwa ujumla wakitakiwa kutumia majukwaa yao kuhubri juu ya umuhimu wa kuwalinda watoto dhidi ya vitendo viovu vya ukatili wa kingono, ikisisitizwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia kuwalinda watoto.   Akizungumza katika ufunguzi wa...